Na Mathias Canal, Rombo
Mbunge wa Jimbo La Rombo ambaye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda leo tarehe 19 Julai 2022 ameanza ziara ya
kikazi ya siku saba jimboni kwake Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Katika ziara hiyo akiwa katika kijiji cha Urauri Kata ya Reha,
Prof Mkenda ameeleza dhamira ya kuwatumikia wananchi katika jimbo lake na
umuhimu wa kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto ya upatikanaji wa
maji safi na salama.
Amesema kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na kampuni ya Kili Water
ilioanzishwa kama kampuni kutoa huduma ya maji Rombo lakini haikuwa na uwezo wa
kutoa maji ya kutosha.
Amesema Wakati huo ilitolewa Bilioni 4 pekee na serikali
kuimarisha upatikanaji wa maji jambo ambalo lililorudisha nyuma ulatikanaji
maji hivyo kutofaa kwa mfumo huo ambapo kulipelekea kuiondoa kampuni hiyo ili
kuimarisha upatikanaji wa maji.
Prof Mkenda amesema kuwa katika hatua za kuimarisha upatikanaji
wa maji serikali iliamua kuanzisha Bodi ya Maji Rombo inayoitwa ROMBOWASA
ambayo inawajibika kutengewa bajeti na serikali kwa ajili ya sekta ya maji.
Mbunge huyo amesema kuwa kufuatia kuanzishwa kwa ROMBOWASA, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 10
kwa wananchi wa Rombo kwa ajili ya upatikanaji wa maji ambapo hadi sasa
wataalamu wanaangalia vyanzo vya maji ili kuhakikisha maji yanafika kwa
wananchi.
"Rais Samia amekuja kuwatumikia watanzania na tayari kwa
sasa ameonyesha njia na ninawahakikishia wananchi tatizo la maji litakamilika
ndani ya muda mfupi" Amekaririwa Prof Mkenda na kuongeza kuwa
"Rais Samia ameamua na amekusudia kuhakikisha maji
yanapatikana na ndugu zangu wananchi nawahakikishia kuwa tuna Rais imara,
mchapa kazi na hata waangusha wanachi wake kamwe"
Prof Mkenda amesema kuwa katika ziara hiyo amekusudia kuwaeleza
wananchi umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na juhudi zinazofanywa na serikali
kupitia Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso za kumtua ndoo mama kichwani.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment