Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Mitawi akiongoza kikao kazi baina ya Watendaji kutoka Ofisi yake, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Elimu, na Taasisi ya Elimu Tanzania chenye lengo la kuweka mikakati ya pamoja ya kuelemisha Umma masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Mitawi ameongoza kikao kazi baina ya Watendaji kutoka Ofisi yake, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Elimu na Taasisi ya Elimu Tanzania kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja katika kuelemisha Umma juu ya masuala ya Muungano.
Katika Kikao kazi hicho kilichofanyika leo Julai 19, 2022 Jijini Dodoma, Bw. Mitawi amesema ni vema jamii ya watanzania ikaelewa kwa kina Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kutazama chimbuko, misingi na maendeleo tangu kuasisiwa kwake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Prof. Makenya Maboko, Dkt. Jennifer Sesabo na Dkt. Aneth Komba Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania wamesema ni vema kitabu hicho cha Muungano sasa kikawa ni sehemu ya mtaala wa kufundishia katika ngazi mbalimbali za elimu, ikiwa ni pamoja na Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
Kitabu cha Historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Chimbuko, Misingi na Maendeleo kimeeleza historia na misingi iliyowezesha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kufanyika, kuimarika na kudumu kwa miaka 58; mafanikio yaliyopatikana pamoja na hoja za muungano zilizojitokeza na hatua zilizochukuliwa kuzipatia katika kuzipatia ufumbuzi.
0 comments:
Post a Comment