METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, July 5, 2022

India Yakusudia kuanzisha Taasisi ya Kiteknolojia nchini Tanzania kufundisha Uhandisi na Teknolojia ya habari-WAZIRI MKENDA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa India nchini Tanzania Ndg Binaya Srikanta Pradhan mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo ofisini kwake Jijini Dar es salaam tarehe 5 Julai 2022. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda akifanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania Ndg Binaya Srikanta Pradhan ofisini kwake Jijini Dar es salaam tarehe 5 Julai 2022. 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akifanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania Ndg Binaya Srikanta Pradhan ofisini kwake Jijini Dar es salaam tarehe 5 Julai 2022. Mwingine pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof James Mdoe (Kulia)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania Ndg Binaya Srikanta Pradhan ofisini kwake Jijini Dar es salaam tarehe 5 Julai 2022. 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda akimsiskiliza kwa makini Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof James Mdoe wakati akifanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania Ndg Binaya Srikanta Pradhan ofisini kwake Jijini Dar es salaam tarehe 5 Julai 2022. 

Balozi wa India nchini Tanzania Ndg Binaya Srikanta Pradhan mbele ya mwenyeji wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda wakati walipokutana na kufanya mazungumzo Jijini Dar es salaam tarehe 5 Julai 2022. 

Na Mathias Canal, WEST-Dar es salaam

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania Ndg Binaya Srikanta Pradhan ofisini kwake Jijini Dar es salaam tarehe 5 Julai 2022.

Katika mazungumzo hayo Balozi Pradhan ameeleza kusudia la Waziri wa Elimu nchini India kumualika waziri Mkenda kuzuru nchini humo ili kujifunza zaidi mambo yahusuyo Teknolojia pamoja na uhandisi.

Waziri Mkenda amemuhakikishia Balozi huyo kuwa atafanya ziara ya kikazi nchini India mapema mwezi Agosti mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mwanzo ya mkakati wa India kuanzisha Taasisi ya Kiteknolojia ya India nchini Tanzania itakayofundisha mambo ya Uhandisi pamoja na Teknolojia ya Mawasiliano.

Waziri Mkenda amesema kuwa Balozi huyo amekwisha kutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kumueleza kusudio hilo hivyo Wizara ya Elimu itatafuta eneo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Taasisi hiyo.

Pia amesema kuwa baada ya kutembelea nchini India atamualika Waziri wa Elimu wa India kuzuru nchini Tanzania kwa ajili ya kutembelea maeneo ambayo yatakuwa yameainishwa kwa ajili ya ujenzi ili kuwa na makubaliano ya haraka ya ujenzi.

Amesema kuwa eneo pekee ambalo Wizara imelifikiria kwa haraka ni Chuo cha Ufundi Dodoma ambacho kitakamilika Disemba mwaka huu na kuanza udahili wa wanafunzi 1500 vilevile chuo cha Tehama ambacho Rais Samia ameagiza kijengwe Jijini Dodoma.

Kadhalika, Waziri Mkenda amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania ingependa kuongeza mahusiano kwenye vyuo vya Ufundi ikiwemo VETA kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi.

Kwa upande wake Balozi wa India nchini Tanzania Ndg Binaya Srikanta Pradhan amesema kuwa Serikali ya India ingependa kwa haraka iwezekanavyo kuanzia mwakani wanafunzi waanze kuchukuliwa kwa ajili ya masomo.

MWISHO

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com