ENG. SALEHE JUMA
ametoa wito huo katika mahafali ya jumuiya ya wanafunzi wa kiislamu wa chuo cha
serikali za mitaa Hombolo mkoani Dodoma ambapo amewasisitiza wahitimu hao kwenda
kutumia elimu yao katika kutoa msaada katika jamii ili elimu yao iwe na tija
chanya kwa jamii.
Aidha ENG.
SALEHE JUMA akatumia fursa hiyo kueleza historia ya Taasisi ya JAI pamoja na
kazi zinafanywa na JAI ikiwemo kusaidia watu wasojiweza, kuhudumia wagonjwa
chakula, kuzika watu ambao hawana ndug pamoja na kuchangia Damu ili kuokoa
maisha ya watu.
Katika hatua nyingine ENG. SALEHE JUMA kwa niaba ya Taasisi ya JAI DODOMA akaadidi Taasisi ya JAI DODOMA kuisaidia jumuiya ya wanafunzi wa kiislamu chuo cha Hombolo mazulia (mikeka) kwaajili ya kufanyia ibada ili kuwawezesha wanafunzi wa chuo hicho kuteleza ibada kwa urahisi.
0 comments:
Post a Comment