CHAMA cha
watu wenye ulemavu Tanzania (CHAWATA) mkoa wa Iringa wameiomba serikali kuweka
mfumo wa elimu jumuishi kwa walemavu ili kutatua changamoto ambazo
wanazokabiliana licha kuwa bado kunachangamoto kubwa ya miundombinu ya elimu
hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali
uliondaliwa na shirika lisilo la kiserikali la IDYDC na kufadhiliwa
na shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa Inclusive Media
Project unaofadhiliwa na Internews Tanzania katika mkoa wa Iringa, Makamu
Mwenyekiti Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) mkoa wa Iringa, Rukia
Makweta alisema kuwa watoto wenye mahitaji maalumu kuchanganyikana na
wengine inatengeneza umoja na kuondoa unyanyapaa kwa kuwa tayari wamezoeana na
kupendana pamoja na kupewa ushirikiano kutoka kwa wenzao..
Makweta alisema kuwa kwa mujibu wa Sheria namba tisa ya watu wenye
ulemavu ya mwaka 2010, inataka haki sawa kwa watu wenye ulemavu ikiwamo elimu,
ajira, nafasi za uongozi na kuboresha miundombinu na kwa mujibu wa jarida ya
Shirika la Kuhudumia watoto Duniani (Unicef), kati ya watoto watano ni wawili
tu wapo shuleni hali ambayo inahitaji elimu jumuishi kuwavutia wengi zaidi.
Aliongeza kuwa katika suala la elimu walemavu wengi
wanakabiliana na miundombinu isiyo rafiki ambayo ni kikwazo katika upataji wa
elimu kwa walemavu waliowengi nchini.
Mmoja ya wanafunzi wenye ulemavu wa kuona, Kephason alisema
shule jumuishi anayosoma bado ina changamoto za kimiundombinu na
kupelekea kuwa na ugumu kutoka sehemu moja hadi nyingine awapo kwenye mazingira
ya shule na kupelekea kukosa ari ya kuendelea na masomo kama wanafunzi wengine
na kuitaka serikali kufanya jitihada madhubuti kurekebisha hili kwani kwa
mwenendo huu wanafunzi wengi wenye ulemavu wanaamua kuacha shule ili kuepukana
na changamoto za kimiundombinu wanazokutana nzao mashuleni kwani huwaathiri
kisaikolojia pia.
“Elimu jumuishi imepewa kipaumbele zaidi kuliko aina nyinginena
inachukuliwa kama njia bora” alisema.
Aidha Makweta alisema kuwa sehemu kubwa ya jamii
nchini imeendelea kukumbatia utamaduni wa kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu
kwa madai mbalimbali ikiwamo ya kuhofia aibu au kuwaona hawatakuwa na uwezo wa
kushiriki shughuli za kijamii ikiwamo elimu.
Naye Katibu wa Shirika la watu wenye Ulemavu, (SHIVYAWATA), Leo
Sambala alisema kuwa moja ya changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni miundo
mbinu isiyo rafiki kwenye shule nyingi za msingi na sekondari ni kati ya
vikwazo vinavyoikabili elimu hiyo mkoani hapo na kuongeza kuwa kama suala
la miundombinu halitapewa uzito, watoto hao watashindwa kujifunza ipasavyo.
“Ni kweli shule zetu zinakabiliwa na miundombinu isiyo rafiki,
hakuna vifaa vya kujifunzia hasa kwa walemavu wasioona, hapa hakuna kujifunza
kwani walemavu wa kutoona wanahitaji vifaa maalum ambavyo sio kila shule
inavyo, kwa hiyo huyu hatajifunza kama ataingia darasani na kukosa vifaa
hivyo.” Alisema Sambala.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Elimu Jumuishi kutoka shirika
lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and
Children Care (IDYDC)linalotekeleza mradi wa Inclusive Media Project mkoa wa
Iringa na kufadhiliwa na Internews Tanzania , Reuben Magayane alisema
kuwa lengo la mradi ni kutumia vyombo vya habari kupaza sauti juu ya
elimu jumuishi na kuibua maswala ya makundi maalumu na walemavu kupitia vyombo
vya habari.
Alisema kuwa jambo ambalo limekuwa halipewi kipaumbele kwenye
vyombo vya habari huku ikiiasa jitihada jumuishi kutoka kwa waandishi wa
habari,jamii na serikai ili kufikia lengo la elimu kwani Msingi wa mafunzo
mbalimbali katika jamii ni chachu ya kuondoa mawazo mgando juu ya watu wenye
mahitaji maalumu kuwa hawawezi, hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kutoa
ushirikiano hitajika kwa watu wenye mahitaji maalumu hasa katika upande wa
elimu.
Alisema
kuwa katika kikao hicho moja ya changamoto ambayo imejitokeza ni ukosefu wa
miundombinu rafiki ya kujifunzia katika shule jumuishi nchini hivyo ni moja ya
njia ambazo zinaathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya wanafunzi na watu
wenye ulemavu.Wilaya ya IringaKwa muda mrefu kumekuwa na kampeni mbalimbali kuhusu
watu wenye ulemavu hasa juu ya haki zao za msingi ikiwamo elimu.
Magayane alisema kuwa kumekuwa na kampeni mbalimbali juu ya watu
wenye ulemavu kupata miundombinu rafiki lakini bado kilio cha watu wenye
ulemavu kupata mahitaji yao muhimu ili waishi kama makundi mengine kwenye jamii
hakikomi.
Aliongeza kuwa changamoto lukuki ikiwamo miundombinu isiyo rafiki kwa wanafunzi wanaoishi na ulemavu, ni moja ya vilio vinavyowafanya baadhi kushindwa kupata elimu na mkoa Iringa ni kati ya mikoa inayokabiliwa na changamoto nyingi katika utoaji wa elimu jumuishi kubwa ikiwa miundombinu isiyo rafiki.
0 comments:
Post a Comment