METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, August 20, 2017

DC MTATURU AONGOZA UZINDUZI WA ALBAMU YA INJILI YA MWIMBAJI ELINEEMA BABU

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa albamu ya tatu ya TARATIBU NITAFIKA iliyoimbwa na Elineema Babu

Katika uzinduzi huo, Mhe.Mtaturu ameendesha zoezi la uuzaji wa albamu hiyo iitwayo TARATIBU NITAFIKA na kusaidia upatikanaji wa zaidi ya shilingi Milioni Tatu ikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi ambapo ofisi yake imechangia jumla ya shilingi milioni moja (1,000,000), huku Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani humo kikiwa kimeunga mkono uzinduzi wa albamu hiyo kwa kuchangia shilingi laki tano (500,000)

Mhe.Mtaturu amewahimiza waimbaji wa nyimbo za injili wilayani humo kutumia vyema fursa waliyonayo kwa kuimba nyimbo zenye kuhamasisha amani na upendo nchini, akitolea mfano kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza iliyoimba wimbo uitwao AMANI kwa ajili ya kuhamasisha amani nchini.

Alisema kuwa tunu ya nchi ya Tanzania ni amani na upendo hivyo wachungaji pamoja na waimbaji wa nyimbo za injili wanapaswa kutilia mkazo uhubiri wao kuhamaisha Upendo, Amani na Mshikamano baina ya wananchi wote pasina kubagua itikadi za kisiasa, dini ama kabila.

Mhe Mtaturu alisema kuwa wanasiasa ambao wamepewa dhamana na wananchi wana jukumu moja la kuwatumikia kwa kuwaletea maendeleo sio kuhubiri siasa na uchochezi jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo yao katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. 

Mwimbaji Elineema Babu ameachia albabu ya tatu iitwayo "Taratibu Nitafika" yenye nyimbo nane ambapo amewasihi wadau wengine kumsaidia kwa kununua albamu hiyo (Audio) ili aweze kupata shilingi Milioni Sita zinazohitaji ili aweze kurekodi video ya albamu hiyo. Taratibu Nitafika ni albamu ya tatu baada ya kutanguliwa na albamu mbili ambazo ni Nitumie pamoja na Fanya Kazi ya Bwana.
Mwimbaji Elieneema Babu akitumbuiza kwenye uzinduzi huo Agosti 20, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mhe. Miraji Mtaturu akionyesha CD alizozindua wakati wa uzinduzi huo ambapo alikuwa mgeni rasmi

DC Ikungi akizindua albamu hiyo

Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe Miraji Mtaturu (kushoto), akimkabidhi CD Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg Philiph Elieza kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji Elineema Babu

Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu (kushoto), akimkabidhi CD Baba Askofu wa Jimbo la Singida Dkt.Paul Samweli

Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe Miraji Mtaturu (kushoto), akimkabidhi CD Mwenyekiti wa mtandao wa Wazo Huru Blog Ndg Mathias Canal kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji Elineema Babu

BMG Habari
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com