Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Queen Sendiga ameagiza uendelezaji wa mradi wa shule ya msingi maalum ya ipogolo ifikapo Augost mwaka huu.
Amesema mkwamo wa jengo la bweni la watoto wenye ulemavu katika shule hiyo unatakiwa kukamilika ndani ya miezi minne na kuitaka Halmashauri ya Manispaa Iringa kuweka mkakati wa kukamilisha mradi huo sambamba na ujenzi wa uzio.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alipokea msaada wa vitanda na magodoro 35 yenye thamani ya shilingi M.4 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye uhitaji maalum katika shule hiyo na kuahidi ukamilishaji wa miundo mbinu ya mabweni hayo ili watoto waweze kuhamia katika mabweni Jambo litakalosaidia wazazi kuendeleza shughuli za kiuchumi na hasa ukizingatia kuwa baadhi yao wametelekezwa na waume zao.
Bi. Elizabeth mmoja wa wazazi wa mtoto anayeosoma katika shule hiyo amesema kutokana na changamoto zinaziwakabili ukiwemo. usafiri na miundombinu mibovu kwa watoto majumbani na mazingira yasiyo salama yanasobabishwa na wao kuwaacha watoto wao walemavu
majumbani pindi wanapokwenda kutafuta mahitaji yao ndiko kunakosababisha shauku yao ya kuiomba Serikali kukamilisha ujenzi huo ili kuwanusuru watoto wao ambao hata huko nyumbani watoto wengine wanalala chini.
Kitengo hicho cha watoto wenye ulemavu wa akili shule ya msingi maalum Ipogolo kilianzishwa Mwaka 2001 ukiwa ni mpango wa Serikali kuwezesha watoto wenye ulemavu wa akili kupata Elimu ambapo kwa Sasa kuna Jumla ya wanafunzi 90, wavulana 66 na wasichana 24 ambapo kati ya hao wengine wako katika elimu jumuishi.
Hata hivyo Afisa Elimu msingi Manispaa Ndugu Charles Mwakalila amesema kwa bajeti inayo anza Julai Mwaka huu zimetengwa milioni 30 kwa ajili ya ukamilishaji wa mabweni na uzio na kwa sasa wadau mbalimbali wameandikiwa barua kuomba kuchangia ujenzi wa jiko na bwalo.
0 comments:
Post a Comment