Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge ameipongeza Halmashauri ya
Wilaya ya Mkalama kwa ukusanyaji wa mapato na hiyo ni kutokana na jitihada
zinazofanyika pamoja na ushirikiano wanaoufanya.
Dk. Mahenge ameyasema hayo leo Juni 14, 2022 kwenye mkutano maalum wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwa ajili ya kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Tarehe 30 Juni 2021 na Tarehe 14 Juni 2022 ambapo alisema katika suala la ukusanyaji
wa mapato hana wasiwasi wala maneno mengi kwa halmashauri hiyo kwani inafanya
vizuri.
“Halmashauri ya Mkalama sina maneno mengi mnafanya kazi vizuri ya
ukusanyaji mapato nina kila sababu ya kuwapongezeni “ alisema Mahenge.
Alisema moja ya kipimo cha kazi nzuri katika halmashauri mbalimbali ipo
kwenye ukusanyaji wa mapato na kuwa mwezi wa tatu mwaka huu
ilifanyika tathmini ya mapato nchi nzima na Mkoa wa Singida kwa bahati mbali
ulikuwa wa mwisho ulikuwa kwenye kati ya asilimia 53 hivi au 54 lakini kati ya
wilaya zaidi ya 70 zilizofanya vizuri moja wapo ilikuwa ni Mkalama na kama
wilaya zingine zingejitahidi tusingekuwa wa mwisho” alisema Mahenge.
Alisema mpaka hivi sasa mavuno mengi ya mkoa wa Singida katika wilaya zote yanafanyika
kuanzia mwezi wa tano na wa sita hivyo wanalazimika kubanana na kuwa anaimani
watafikia asilimia 80 huku Mkalama wakiwa asilimia 95 hivyo niendelee kuwaamini
leo ni tarehe 14 zimebaki wki mbili mkihimarisha ukusanyaji wa mapato katika
mageti tutafikisha asilimia 100.
Katika hatua nyingine Mahenge ameendelea kupiga marufuku watu wanaojiita
waganga wa kienyeji ' maarufu kama rambaramba) ambao wamekuwa wanapiga ramli chonganishi na kuchangisha fedha
wakidai wanatoa uchawi na kutishia amani ndani ya wilaya hiyo kuwa waache mara moja kufanya hivyo vinginevyo watakamatwa
na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo alisema mpaka hivi sasa katika
ukusanyaji wa mapato wamefikia asilimia 95, jumla ikiwa ni asilimia 98 na kuwa
kama mvua zingekuwa zimenyesha vizuri wangekuwa wanazungumzia asilimia 120 na kueleza kuwa ukusanyaji huo umefia hatua hiyo kutokana na kazi nzuri wanayoifanya
madiwani.
“Mheshimiwa mkuu wa mkoa najisikia vizuri sana kwa kazi wanayoifanya hawa
madiwani kwa kweli wananiheshimisha na wanafanya kazi nzuri” alisema Kizigo.
Diwani wa Kata ya Nkindo Reuben Muhai alisema watendaji wote wanaosimamia
ukusanji wa mapato wasing’ang’anie kukaa kwenye mageti badala yake waende
kutafuta vyanzo vingine vya mapato vitakavyosaida kuiongezea halmashauri hiyo
mapato.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Singida kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG) Othman Jumbe alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos na wenzake kwa kufanya kazi nzuri na kuwa
ofisi ya CAG na wao lengo lao ni moja la kuhakikisha halmashauri hiyo inasonga
mbele.
Alisema ukaguzi walioufanya mwaka juzi miradi mingi ilikuwa bado
haijakamilika lakini kwa ukaguzi mwingine uliofanyika imeonesha miradi yote
imekamilika hivyo anakila sababu ya kuwapongeza na kuwa viongozi wa wilaya hiyo
wapo vizuri katika kufuatilia miradi na ukamilikaji wake na akatumia nafasi
hiyo kuzungumzia umuhimu wa kuwa na lisiti baada ya kufanya manunuzi mbalimbali
kwani lengo ni kuhakikisha kila mfanya biashara analipa kodi ya Serikali.
Katika kikao hicho hoja mbalimbali za CAG zilipitiwa na kujadiliwa na waheshimiwa madiwani ambapo Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Bosco Samwel aliwaomba madiwani hoja zote zilizokwisha jadiliwa zisipelekwe tena kwenye kikao kijacho bali zile za sera.
0 comments:
Post a Comment