Mbunge wa Kavuu na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe Geophrey Pinda amewataka Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha wanaboresha barabara jimboni kwake hasa kipindi hiki cha mavuno.
Mhe Pinda ametoa rai hiyo wakati akitembelea na kukagua barabara mbalimbali jimboni kwake wakati huu wananchi wakiwa wamevuna mazao yao na yanatakiwa yatoke shambani na kwenda sokoni.
“Tumehamasisha wananchi wakalima kwa wingi sana lakini baadhi ya sehemu miundombinu ya barabara imeharibika na tungependa kuwaomba TARURA kuweza kutuangalia na kuhimarisha sana barabara zetu hizi hasa kipindi hiki cha mavuno,” amesema Mhe Pinda.
0 comments:
Post a Comment