Na Mathias Canal, WEST
Serikali
imesema kuwa ina mpango kabambe wa kukimbiza na kuyafanyia haraka mageuzi ya
elimu ambapo kufikia mwezi Disemba 2022 rasimu ya Mitaala mipya pamoja na
rasimu ya mapitio ya sera itakuwa imekamilika.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe
18 Mei 2022 Ofisini kwake Jijini Dodoma wakati alipokutana na kuzungumza na Mwakilishi
Mkazi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa Bw Zlatan Milisic.
Waziri
Mkenda amemuhakikishia mgeni wake kuwa serikali ya Tanzania imejipanga vyema na
kufikia Mwezi Januari mwaka 2023 inatarajia kuanza mchakato wa kufanya maamuzi
baada ya Rasimu hiyo kuwa imekamilika.
Waziri
Mkenda ameeleza kuwa Umoja wa Taifa umeandaa mkutano maalumu unaotarajiwa
kufanyika mwezi Septemba mwaka huu Mjini New York nchini Marekani kujadili mageuzi
makubwa ya elimu Duniani.
Waziri
Mkenda ameeleza kuwa Mkutano wa wakuu wa nchi utaanzisha mchakato katika nchi
nyingi Duniani lakini wakati zinaanza mageuzi hayo ya elimu tayari Tanzania
itakuwa imefikia hatua nzuri za maamuzi hivyo kwenda mbele kwa haraka Zaidi.
Prof
Mkenda amesema kuwa mchakato huo wa magezi hayo nchini Tanzania umetokana na maagizo
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan aliyotoa
wakati akilihutubia Bunge la Tanzania tarehe 22 Aprili 2021 kuhusu mabadiliko
ya Mitaala ya elimu na muelekeo mpya katika sekta ya elimu aitakayo.
“Na
mimi niwahakikishie tu kuwa Kupitia umoja wa Mataifa ni rahisi kujua nchi
zingine zinafanya nini kwenye sekta ya elimu ili kuweza kuboresha sekta yetu”
Amekaririwa Prof Mkenda na kuongeza kuwa
Amemuahidi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda kuendeleza
ushirikiano ili kuhakikisha kuwa malengo ya maboresho kwenye elimu yanatimia
ili elimu itolewayo iendelee kuwa bora.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment