METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, April 27, 2022

SERIKALI KUFUFUA SHULE ZA MSINGI ZA UFUNDI WILAYANI HAI-WAZIRI MKENDA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akijibu maswali bungeni Jijini Dodoma wakati wa mjadala wa bajeti leo tarehe 27 Aprili 2022. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akijibu maswali bungeni Jijini Dodoma wakati wa mjadala wa bajeti leo tarehe 27 Aprili 2022. 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akijibu maswali bungeni Jijini Dodoma wakati wa mjadala wa bajeti leo tarehe 27 Aprili 2022. 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe Saasisha Mafuwe wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni Jijini Dodoma wakati wa mjadala wa bajeti leo tarehe 27 Aprili 2022. 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akiwasili bungeni Jijini Dodoma wakati wa mjadala wa bajeti leo tarehe 27 Aprili 2022. 

Na Mathias Canal, Dodoma


Serikali ipo katika mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) na uboreshaji wa Mitaala ya Elimu ili iweze kuwajengea wanafunzi stadi na ujuzi mbalimbali ikiwemo ufundi utakaowawezesha wahitimu kuhimili ushindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.


Mara baada ya mitaala tajwa kukamilika ikiwa ni pamoja na manunuzi ya vifaa na mashine mbalimbali za ufundi, Elimu ya Ufundi itatolewa katika Shule za Msingi na Sekondari. Aidha, utaratibu wa kufanya mitihani ya Elimu ya Ufundi na kupata vyeti utaandaliwa kwa kushirikiana na mamlaka husika kama vile Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 27 Aprili 2022 bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Hai Mhe Elinikyo Mafuwe Saashisha aliyetaka kufahamu serikali ina mpango gani kufufua Shule za Msingi za Ufundi zilizopo Wilaya humo pamoja na kuweka utaratibu kwa Wanafunzi wa Shule hizo kufanya mitihani na kupata Vyeti.


Waziri Mkenda amesema kuwa pamoja na mapitio ya Sera na Mitaala, Serikali inaendelea kufanya maboresho makubwa katika Chuo cha Ualimu Kleruu pamoja na Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Morogoro (MVTCC) kwa kufanya ukarabati wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa mabweni ya Wanafunzi kwa lengo la kuongeza fursa ya mafunzo kwa Walimu wa masomo ya Ufundi.


Ameongeza kuwa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kimeanza maandalizi ya utoaji wa mafunzo hayo katika ngazi ya Stashahada katika Elimu ya Ufundi (Diploma in Technical Education) na Postgraduate Diploma in Technical Education. “Kwa sasa Mitaala ya Masomo hayo inafanyiwa kazi na Tume ya Vyuo Vikuu ili kuidhinishwa na kuanza kutumika katika Chuo hicho” Amekaririwa Prof Mkenda


MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com