METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, April 25, 2022

OFISI YA RC SINGIDA, BODI YA KOROSHO WAKUTANA KUMALIZA CHANGAMOTO YA WAKULIMA WA KOROSHOMANYONI

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge akiongoza kikao cha kutatua changamoto iliyojitokeza baada ya wakulima waliolipia mashamba kwa ajili ya kilimo cha korosho wilayani Manyoni mkoani hapa kutopatiwa mashamba yao kwa zaidi ya miaka mitatu. Kikao hicho kilichowahusisha viongozi wa juu wa Bodi ya Korosho Tanzania kilifanyika jana wilayani humo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu  Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred akizungumza kwenye kikao hicho. 

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Wakulima wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Taswira ya kikao hicho.
Mkulima Michael Sanga akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkulima Lusekelo Nkuwi akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkulima Titus Mwisomba akitema nyongo kufuatia madhira aliyopata na wenzake katika kufuatilia mashamba hayo.
Mkulima Abdalla Mbonde akielezea madhira waliyopata kufuatilia haki yao baada ya kulipia mashamba hayo ambayo hadi leo hii bado hawajapatiwa
Mwakilishi wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) 834 Deti Mkiwa akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkulima Mdachi Chande kutoka Kata ya Mkwese akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkulima Sabastiani Kandila akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkulima Halima Nassoro akizungumza kwenye kikao hicho.
Wakulima wakiangalia orodha ya majina yao yaliyobandikwa nje ya ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kujua wapo katika kundi gani kati ya wakulima waliopata mashamba hayo au laa.

Na Dotto Mwaibale, Manyoni

OFISI ya Mkuu wa Mkoa Singida na Bodi ya Korosho Tanzania  (CBT) wamekutana wilayani Manyoni mkoani  hapa kutatua changamoto ya wakulima ambao walilipa fedha zao miaka mitatu iliyopita  kwa ajili ya kilimo cha zao la korosho katika wilaya hiyo lakini hadi leo hii bado hawajapatiwa mashamba yao.

Kikao hicho kinafanyika kufuatia agizo la Waziri wa Kilimo alilolitoa Aprili 9 mwaka huu kutaka wakutane wakulima hao, bodi ya korosho na ofisi ya mkuu wa mkoa  ili kumaliza sintofahamu ya jambo hilo

Mashamba waliotakiwa kupewa yapo Itigi-Njilii, Kaminyange, Masigati na Mkwese ambapo kuna makundi manne ya wakulima ambao wapo kwenye mgogoro huo ulianza kutatuliwa na Serikali mkoani hapa kwa kushirikiana na bodi ya korosho.

Makundi hayo ni la wakulima ambao walilipia mashamba hayo na wameanza kulima, wapo wenye mashamba lakini ni mapori, wapo wenye mashamba lakini hawajakabidhiwa rasmi na wale ambao walilipia lakini wapowapo tu na hawajui hatima yao.

Katika kikao hicho baadhi ya wakulima walipewa  nafasi ya kujieleza na kutoa masikitiko yao ya kupoteza muda mwingi wakisumbuliwa kwa zaidi ya miaka mitatu bila ya kupewa mashamba hayo licha ya kutoa fedha zao Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge alisema maazimio yaliyofiwa ni ndani ya mwezi mmoja mvutano huo uwe umemalizika na kabla ya Oktoba 1, 2022  wakulima wote waliolipia fedha zao na kukamilisha taratibu zote wakabidhiwa mashamba yao na kuanza kulima.

Alitaja jambo lingine kuwa kutumika kwa akaunti moja ya mradi huo na kuundwa kwa kamati mpya itakayosimamia baada ya zile mbili za awali kuvunjwa na kuomba wahusika wa kamati hizo zilizovunjwa kutoa ushirikiano kwa kamati mpya na watakaoonekana wanashindwa kutoa ushirikiano watachukuliwa hatua.

Alisema suala hilo litasimamiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko kwa kushirikiana na kamati itakayoundwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania, Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile aliwashukuru wajumbe wa kikao hicho kwa kuwa wawazi  na kueleza kuwa kilikuwa kikao cha kujua changamoto zilizokuwepo.

Alisema jambo lililomtia moyo ni hatua aliyoichukua mkuu wa mkoa na timu yake yakulimaliza jambo hilo ndani ya mwezi mmoja na kuwa kilimo cha zao hilo licha ya kupunguza umasikini wa mtu mmoja mmoja kinakwenda kuongeza pato  la taifa hivyo aliwasihi baadhi ya wakulima waliofikia hatua kudai warudishiwe fedha zao kuacha kufanya hivyo na akasema watendaji wote waliohusika kwa namna moja hama nyingine kuchangia changamoto hiyo wamesamehewa.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu  Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred akizungumza kwenye kikao hicho alisema tayari baadhi ya kazi alizoagizwa kuzitekeleza kama ujenzi wa kisima cha maji baridi kwa ajili ya kumwagilia miche ya korosho watakayokuwa wakiizalisha Naliendele Mtwara mchakato wake umefanyika ukiwepo wa ujenzi wa ghara la kisasa la kuhifadhi korosho litakalo jengwa wilayani Manyoni.

Mkulima Abdallah Mbonde akizungumza kwa niaba ya wenzake ameshauri kamati itakayoundwa ihakikishe haki inatendeka ili wakulima waweze kuendelea na uwekezaji katika kilimo hicho kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com