Na Fredy Mgunda,Iringa
JUMLA ya bilioni 2,169,161,640 zimetumika katika ujenzi na kukarabati barabara za wilaya ya Iringa zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 kwa lengo la kuwarahisishia wananchi usafi na kusafirisha mizigo ambayo inasaidia kukuza uchumi.
Akizungumza wakati wa kukagua miradi ya barabara wilaya ya Iringa,meneja wa TARURA wilaya ya Iringa Eng Barnaba Jabiry alisema kuwa barabara hizo zimejengwa kwa kutumia fedha ya tozo za mafuta.
Eng Jabiry alisema kuwa fedha hizo za tozo zimetolewa na serikali kwa lengo la kuwarahisishia wananchi usafi ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi kwa wakati na kupata maendeleo yanayostahili.
Alisema kuwa barabara zilizojengwa ni barabara ya Ikengeza Nyang'oro yenye kilometa 10 kwa gharama ya shilingi milioni 264,049,000 kwa kiwango cha changarawe,matengenezo makubwa ya barabara ya Ikengeza Igodikafu iliyogharimu kiasi cha 396,279,000.
Eng Jabiry aliongeza kuwa wamefanikiwa kufanya matengenezo ya barabara ya Malizanga kilimeta 2,matalawe kilimeta 2,Mapogoro Kitisi kilometa 4.25 Makombe kilometa 2,Kitanewa kilometa 5, pamoja na ujenzi wa Daraja mfuto barabara ya Wasa Mahuninga ampo zimetumia kiasi cha shilingi milioni 279,638,700.
Aidha ENG Jabiry alisema kuwa wanaendelea na ujenzi wa dharura wa daraja la TAO katika barabara ya Kitayawa na Lupembelwasenga ambalo lilisombwa na maji kutoka na kunyesha kwa mvua nyingi za masika na daraja hilo litagharimu kiasi cha shilingi milioni 123,265,000.
Alisema kuwa katika wilaya ya Iringa wamefanya matengenezo na ujenzi wa barabara ya Kibena Mfukulembe yenye kilometa 5.06,matengenezo ya kawaida ya barabara ya Ilandutwa Ifunda kilimeta 3,Udumka Igomtwa kilimeta 2 kwa gharama ya shilingi milioni 110,085,000 na matengenezo maalum ya barabara ya Ifunda Bandabichi Itengulinyi kwa gharama ya shilingi yalingi milioni 984,238,710.
Eng Jabiry alimazia kwa kusema kuwa kukamilika kwa barabara hizo kutachochea
maendeleo ya wananchi kwa kukuza uchumi kutoka na kurahisishiwa usafiri na
serikali.
kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga aliwataka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Iringa kuhakikisha wanawashirikisha viongozi wa maeneo husika wakatia wa ujenzi na ukarabati wa barabara hizo.
Sendiga alisema kuwa wananchi wamekuwa wanaharibu miundombinu ya barabara kutokana na kutokuwa na elimu ya umuhimu wa barabara hizo hivyo ni muhimu kwa TARURA kutoa elimu kwa wanachi jinsi ya kuzitunza barabara hizo.
Alisema kuwa ni muhimu kuendelea kuwasimamia wakandarasi ili wamalize kazi kwa wakati unaotakiwa na ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha ambayo imetolewa na serikali.
Lakini Sendiga aliwaagiza viongozi wa TARURA kuhakikisha kila barabara inayojengwa inakuwa na mitaro ambayo itapitisha maji ili kuzilinda barabara zisiaharibike mapema.
Sendiga alisema kuwa anawapongeza TARURA wilaya ya Iringa kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusimamia wakarandarasi kufanya kazi kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha husika
0 comments:
Post a Comment