Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa akionyesha misokoto bangi Iliyokamatwa na jeshi la polisi katika Msako wa April 10 na 12 mwaka huu.
![]() |
Misokoto ya bangi iliyokamatwa kwa mwanamke mfanyabiashara wa madawa hayo mkoani singida |
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa akiwaonyesha waandishi wa habari misokoto ya bangi |
ACP Stella Mutabihirwa akiaangalia misokoto ya bangi wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya kuwakamata wahalifu wanajihusisha na biashara hiyo. |
![]() |
Madumu ya mafuta ya Dizeli lita 300 aliyokuwa akiyaiba kwenye magari makubwa yaliyokamatwa kwa mtuhumiwa ajulikanaye kama Emanuel Juma (29) mkazi wa Ulyampiti wilaya yaIkungi mkoani Singida. |
Na Hamis Hussein - Singida
JESHI
la Polisi Mkoani Singida Katika misako na oparesheni iliyofanya kuanzia april
mosi hadi 16 mwaka huu limebaini matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo ni wizi
wa mafuta ya dizeli pamoja na umiliki wa misokoto ya bangi katika maeneo ya
kadhaa ya mkooni hapa.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Stella
Mutabihirwa amesema jeshi hilo linamshikilia mwanamke mmoja wa umri wa miaka 29
ambaye jina lake limehifadhiwa mkazi wa
Mnung’una kata ya minga wilaya ya
Singida baada ya kukutwa na bangi ambapo
amekuwa akijihusisha na uuuzaji wa madawa hayo ya kulevya ambapo ameonekana
kuwa akifanya biashara ya kuuuza bangi wa watu .
ACP
Mutabihirwa alisema kuwa Mwanamke huyo alikuwa na misokoto 1948 ya bangi sawa
na kilogramu kumi na tayari anashikiliwa
kwa uchunguzi zaidi ili kubaini mtandao mzima wa wauzaji wa madawa ya
kulevya mkoani hapa .
“Tulifanikiwa kumkamata mwanamke mmoja siku
ya tarehe 10 mwezi wa nne ambaye jina lake tumelihifadhi ni mwanamke mwenye umri
wa miaka 29, alikamatwa katika maeneo ya Mnung’una kata ya Minga Wilaya ya Singida.
Mwanamke huyu amekuwa akijihusisha na uuzaji wa bangi na alikutwa na misokoto
ya bangi 1948 sawa na kilogram 10 alizokuwa amezihifdhi kwenye salfeti kwa
lengo la kuisambaza na kuiuza katika mkoa wetu wa singida” . Alisema Kamanda ACP Mutabihirwa.
Kamanda
ACP Stella Mutabihirwa aliongeza kuwa katika oparesheni ilifanyika april 12
jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mwingine aliyekutwa na misokoto 671
sawa na gramu 2 ambazo alikuwa amezihifadhi kwenye salfeti na na kwamba jeshi
hilo bado linaendelea na msako kubaini mtandao mzima wa wasambazaji wa madawa
ya kulevya ndani ya mkoa wa Singida.
Katika
Msako wa jeshi hilo mnamo april 9 mwaka huu katika kijiji cha Ulyampiti wilaya ya Ikungu liliweza kumkamata mtuhumiwa mmoja aliyejulikana kwa jina la Emanuuel
Juma mwenye umri wa miaka 29 akiwa na mafuta ya Dizeli lita 300 ndani ya
madumu 18 ya lita 20.
ACP
Stella alisema mtuhumiwa huyo (Emanuel) alikuwa akiiba mafuta kwenye magari
makubwa yapitayo Ikungi mkoani hapa kisha kuchukua mafuta na kuwauzia wananchi
kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta nchini na katika soko la dunia.
“Katika msako wa jeshi la polisi wa april
9 mwaka huu tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa wizi wa mafuta ya dizeli,Tulipata
taarifa kuwa kuna mwananchi mmoja anafahamika kwa jina la Emanuel Juma mwenye
umri wa miaka 29, anajihusisha na wizi wa mafuta ya Dizeli katika magari
makubwa amabyo yanayopita hapo Ikungi kwahiyo aliweza kuhifadhi lita 300 za
dizeli nyumbani kwake na kutokana na kupanda
kwa bei ya mafuta amekuwa akiwauzia watu kwa bei ya nchini” alisemea ACP Mutabihirwa.
Kuhusu
sikukuu ya Pasaka Kamanda Mutabihirwa aliwataka wakazi wa mkoa wa Singida
kusherekea kwa amani ambapo aliwataka
wazazi na walezi kuhakikisha wanaacha watu majumbani ili kuwa walinzi wa miji
yao pindi watakapokuwa katika nyumba za ibada pamoja na maeneo ya kusherekea na
kuongeza kuwa jeshi hilo litaendelea na doria za miguu , magari pikipiki na
doria za mbwa kama ulivyo utaratibu wao
ili kuhakikisha mkoa wa Singida unakuwa salama wakati huu wa kusherekea sikukuu hiyo.
0 comments:
Post a Comment