METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, March 18, 2022

WAZIRI MKENDA AAGIZA KUFANYIKA MKUTANO WA UCHAGUZI WA SCAUTI TANZANIA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi na kamati tendaji ya Scauti Tanzania akiwa ameambatana na Scauti Mkuu Tanzania Bi Mwantumu Maiza kilichofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es salaam leo tarehe 18 Machi 2022. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Wajumbe wa kamati tendaji ya Scauti Tanzania wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi na akiwa ameambatana na Scauti Mkuu Tanzania Bi Mwantumu Maiza kilichofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es salaam leo tarehe 18 Machi 2022.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi na kamati tendaji ya Scauti Tanzania akiwa ameambatana na Scauti Mkuu Tanzania Bi Mwantumu Maiza kilichofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es salaam leo tarehe 18 Machi 2022.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda na Scauti Mkuu Tanzania Bi Mwantumu Maiza wakiwa katika picha ya pamoja na kamati tendaji ya Scauti Tanzania mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi kilichofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es salaam leo tarehe 18 Machi 2022.
Wajumbe wa kamati tendaji ya Scauti Tanzania wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi na akiwa ameambatana na Scauti Mkuu Tanzania Bi Mwantumu Maiza kilichofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es salaam leo tarehe 18 Machi 2022.

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda ameteua kamati ya mpito ya watu watatu ambayo itashughulikia shughuli za kiutendaji za Scauti Tanzania.

Kamati hiyo tendaji pia imepewa jukumu la kuhakikisha inaandaa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa uongozi wa Scauti.

Ameitaka kamati hiyo ya mpito kuhakikisha kuwa inatoa Notisi tarehe 21 Machi 2022 na kuagiza mkutano mkuu ufanyike ndani ya siku 60 mara baada ya tangazo hilo.

Waziri Mkenda ametoa agizo hilo leo tarehe 18 Machi 2022 wakati wa kikao kazi na kamati tendaji ya Scauti Tanzania akiwa ameambatana na Scauti Mkuu Tanzania Bi Mwantumu Maiza kilichofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es salaam

Waziri Prof Mkenda amesema kuwa kamati hiyo tendaji itaongozwa na Bw Stewart Kiluswa akisaidiana na Omary Mavura pamoja na Suleiman Takadiri

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com