METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 16, 2022

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI YA WATU WENYE ULEMAVU IKULU CHAMWINO, MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Heshima kutoka Bi. Nuru Awadh kwa niaba ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania kabla ya kuzungumza na Makundi hayo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Machi, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua juu Tuzo ya Pongezi mara baada ya kukabidhiwa kutoka kwa Watu wenye Ulemavu Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Machi, 2022. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makundi mbalimbali ya watu wenye Ulemavu, Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu (SWAUTA), Shirikisho la Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu SHIVYAWATA, katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Machi, 2022. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Pongezi kutoka kwa Watu wenye Ulemavu Tanzania kutoka kwa Stella Jailos wa SWAUTA kabla ya kuzungumza na Makundi hayo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Machi, 2022. 

Makundi mbalimbali ya burudani ya Watu wenye Ulemavu wakitoa burudani katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Machi, 2022.

Makundi mbalimbali ya watu wenye Ulemavu, Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu (SWAUTA), Shirikisho la Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu SHIVYAWATA, wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiwahutubia katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Machi, 2022.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com