JABIR
SHEKIMWERI ametoa rai hiyo katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma
alipowatembele wagonjwa kuwajulia hali na kuwapatia huduma ya uji iliyoandaliwa
na Taasisi ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI) mkoa
wa Dodoma ambapo ameisisitiza JAI kujikita katika utoaji elimu ya lishe ili
kusaidia kuondoa tatizo la utapiamlo kwa wakazi wa jiji hilo .
Aidha JABIR SHEKIMWERI amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana
na Taasisi hiyo ya (JAI) na kuahidi kuipatia taasisi hiyo eneo la uwanja kwa
ajili ya ujenzi wa ofisi za taasisi hiyo haili itakayosaidia (JAI) kuendelea
kutoa huduma katika jamii
Kwa upande
wake Amiri wa Taasisi ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI) mkoa
wa Dodoma ALLY KANDA akaeleza huduma zinazotolewa na taasi hiyo katika jamii ikiwemo kuwalisha wagonjwa,kuwasaidia huduma
za dawa na kusafirisha kwenda makwao.
Naye Mratibu wa Taasisi hiyo ya Taasisi ya Jamiiyatul
Akhlaaqul Islaam (JAI) mkoa wa Dodoma MOHAMEEDI OTHUMANI akatumia fursa hiyo
kueleza changamoto zinazoikabili taasisi hiyo ikiwemo ukosefu wa ofisi huku
akiiomba serikali kuiwezesha Taasisi hiyo kuweza kupata ofisi.
0 comments:
Post a Comment