METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, March 15, 2022

FINA kutoa Ufadhili wa Masomo na mafunzo ya Mchezo wa Kuogelea



Waziri wa utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la  Mchezo wa Kuogelea duniani (FINA) Husain AL Musallam, na kukubaliana Shirikisho hilo  kusaidia ufadhili wa masomo na mafunzo ya mchezo wa kuogelea nje ya nchi kwa vijana wawili wa kike na wa kiume.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Machi 15, 2022 mjini Zanzibar,Mhe. Mchengerwa amesema, FINA itasaidia upatikanaji na uboreshaji wa miundo mbinu ya mchezo wa kuogelea hapa nchini.

Kufuatia fursa hiyo, Waziri Mchengerwa amemwagiza mkurugenzi wa Michezo nchini Yusuph Singo, kuhakikisha anasimamia kwa ukaribu na ufanisi mchakato mzima wa kuwapata vijana watakao pelekwa masomoni kupitia ufadhili huo ili kutenda haki na kuwapata vijana wenye sifa, uwezo na kiu ya kufanya vizuri katika mchezo wa kuogelea.

Kwa upande wake Rais wa FINA Al Musallam ameeleza kufurahishwa kwake na mapokezi aliyopata tangu alipowasili hapa nchini  kukagua maendeleo ya Mchezo wa Kuogelea na kuahidi kuongeza ushirikiano zaidi kadri serikali itakavyokuwa tayari kushirikiana na FINA katika masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha mchezo huo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com