METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, February 8, 2022

TANZANIA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA-WAZIRI MCHENGERWA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa (mwenye kofia nyeupe)  na Balozi wa Qatar nchini(mwenye kofia) wakikabidhi kombe  kwa  wachezaji wa timu ya Shirika la ndege la Qatar  baada ya kuifunga 8-2 timu ya watumishi wa ubalozi wa Qatar kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya michezo ya nchi hiyo jijini Dar es salaam.

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa kitoa hotuba kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya michezo ya nchi ya Qatar Februari 8, 2022 jijini Dar es salaam.

VIONGOZI  wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Viongozi wa Ubalozi wa Qatar katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa hafla ya kuadhimisha siku ya michezo ya nchi ya Qatar Februari 8, 2022 jijini Dar es salaam.

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Qatar Hussain bin Ahmad Al Homaid kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya michezo ya nchi ya Qatar Februari 8, 2022 jijini Dar es salaam.

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania inatarajia kushiriki kwenye mashindano ya kombe la dunia baada ya kumalizika mashindano ya mwaka huu 2022 yanayofanyika Qatar kutokana na mikakati kabambe ya maandalizi inayoendelea hizi sasa.

Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Februari 8, 2022 jijini Dar es Salaam kwenye halfa iliyoandaliwa na ubalozi wa Qatar, kuadhimisha siku ya michezo ya nchi hiyo inayofanyika kila jumanne ya mwezi Februari kila mwaka.

Katika halfa hiyo aliambatana ya Katibu Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha.

Amesema Tanzania inakusudia kushiriki katika mashindano hayo kutokana na mikakati kabambe iliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya michezo nchi nzima.

“Sisi kama taifa ni muhimu tukubali ili kufanikisha zoezi hili la kushiriki ni  mashindfano makubwa kama haya  lazima kujiandaa  na kuboresha  miundo mbinu ya michezo ambapo  kwa sasa  tumeshatenga shule 56 nchi nzima  kwa ajili ya michezo”. Amefafanua Mhe, Mchengerwa

Aidha, amesema Serikali inakusudia kujenga viwanja vikubwa vya ndani ambavyo vinajumuisha michezo mbalimbali viwili kwenye mji wa Dar es Salaam na Dodoma pia tunatarajia kujenga maeneo makubwa ya burudani tatu

Amemwomba Balozi wa Qatar Mhe. Hussain Bin Ahmad Al Homaid kuiomba Serikali ya nchi yake kuisaidia Tanzania kwenye eneo la miundombinu ili kuendelea kuimarisha uhusiano uliojengeka baina ya nchi hizo mbili.

Amemhakikishia Balozi kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ipo tayari kuendelea kushikiana wakati wowote kwenye sekta za michezo, Sanaa na Utamaduni kwa faida ya wananchi wa nchi zote mbili.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Al Homaid ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwa na uhusiano mzuri na nchi yake na kuahidi kuendelea kufanya hivyo.

Pia amesema nchi yake imeitenga siku hii ya michezo ili kuendeleza michezo na kuwafanya wananchi wake kuepukana na kupatwa na magojwa yanayoweza kuzuilika kwa kufanya mazoezi.

Amesema kuwa nchi yake inakwenda kuwa nchi ya kwanza miongoni mwa nchi za kiarabu kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia.

Katika Hafla Mhe. Mchengerwa na Balozi  Al Homaid walipiga mpira wa miguu golini kuashiria ufunguzi rasmi wa siku hiyo huku timu ya ubalozi huo na ile ya watumishi wa shirika la ndege la nchi hiyo walicheza  mechi ya kirafiki na timu ya ubalozi kufungwa mabao 8-2 dhidi ya timu ya Shirika la ndege la Qatar.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com