Na Mwandishi wetu
Dodoma
MBUNGE
wa Viti Maalum (CCM) Bahati Ndingo ameihoji serikali Bungeni kuhusu mpango
uliopo wa kutenga fedha za ukarabati wa vituo vya wazee ambavyo vingi
vimechakaa.
Bahati
aliuliza swali hilo jana Bungeni kwa Naibu Waziri, Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum, Mwanaidi Ali Khamisi.
Akijibu
swali hilo, Mwanaidi alisema katika kuboresha utoaji wa huduma, serikali
imeendelea kuboresha majengo na miundombinu ya makazi ya wazee kwa awamu ambapo
kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 na mwaka wa fedha 2020/2021 ukarabati
umefanyika katika makazi saba ya wazee yakiwemo Nunge (Dar es Salaam),
Kolandoto (Shinyanga), Njoro (Kilimanjaro), Magugu (Manyara), Kiilima (Kagera),
Fungafunga (Morogoro) na Sukamahela (Singida).
Aidha,
alisema serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa Makazi ya
Wazee Wasiojiweza nchini kwa kadri ya upatikanaji wa rasilimali fedha.
Hata
hivyo, Mbunge Bahati alipata nafasi kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza
ambapo katika swali lake la kwanza alitaka kufahamu mpango wa serikali wa
kuongeza idadi ya vituo vya kulelea wazee.
“Tafiti
mbalimbali zimeonyesha uwepo wa ongezeko la wazee duniani, je, wizara inajipangaje
kuongeza idadi ya vituo vya kulelea wazee,” alihoji.
Kadhalika,
katika swali lake la pili, alihoji mpango wa serikali wa kuweka vifaa tiba
katika vituo mbalimbali vya kulelea wazee.
Akijibu
maswali hayo, Mwanaidi alisema kila mwaka wa fedha serikali imekuwa ikitoa
fedha kuboresha mahitaji ya wazee kama mavazi, chakula na afya bora.
Alisisitiza kuwa serikali ya Rais Samia inawajali na kuwathamini wazee kwa kuhakikisha kundi hilo muhimu linapata huduma bora.
0 comments:
Post a Comment