METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, February 15, 2022

DKT. BITEKO KUONGOZA KONGAMANO LA SEKTA YA MADINI IRAMBA -SINGIDA | WADAU WAJITOKEZA KWA WINGI KUSHIRIKI



Waziri wa Madini Mhe. Dk. Doto Biteko, anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la madini litakalofanyika Wilaya ya Iramba mkoani hapa Februari19, 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba , Mhe. Suleiman Mwenda, Mratibu na Mwenyeji wa kongamano  la Sekta ya Madini Wilayani Hapo akiwa ofisini kwake baada ya kuzungumza na waandishi wa habari.


Jiwe la Dhahabu ikiwa ni moja ya Malghafi za Madini


Baadhi ya Wachimbaji wa Madini waliowahi kushiriki Mikutano na Wadau wa Madini  


Na, Hamis Hussein-Singida

SEKTA ya Madini inatarajia kufanya Kongamano na wadau madini Mkoani Singida ambalo litakalofanyika Febuari 19, 2022 wilayani Iramba Mkoani  hapa na tayari maandalizi kuelekea kongamano hilo yamepamba moto baada ya wadau mbalimbali kujitokeza kushiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda alisema maandalizi hayo yanaendelea vizuri na kuwa wadau wengi wa maendeleo wilayani humo wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kushiriki kongamano hilo ambalo ni la muhimu katika kuinua uchumi wilayani humo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko.

"Wadau tuliowaandikia barua kuwaomba watusaidie katika michango ya kuandaa kongamano ili ni wengi na wameonesha kukubali kushiriki" alisema Mwenda.

Mwenda aliwataja wadau hao kuwa ni NSSF,Benki ya CRDB, NMB,TCB,Exim,NBC,Microfinance–Maboto,Faniki,Faidika,AB One, Lekima, Werema, Chogo, BankABC na zingine zilizopo Iramba.

Aliwataja wadau wengine kuwa ni NHIF,Migodi –Sunshine, Sekenke One, Dealers Soko la Shelui , Nabii Elia Makuli, Mgodi wamchongomani ( UWAWAKI SHE) , UWEMA, UWASEKE, Alex Odipo na WAshirika (Mgodi wa Mbuyuni), Yahya Mshokela na Washirika (Mgodi wa Shinyanga), Yudathadei Alex Massawe, Ekarist Kiwia, Nestory Jalima, Daniel Zulungu, Aisha Kamrudi ni Mohommed, Mohammed Sombida Mchina, Philbert Adrian, Sechu Gast on, Waziri Hussein, John Bina Wambura, Peter Bina Wambura, Gihoni Investment na Javan Investment C.Ltd.

Aidha Mwenda alitaja waalikwa kuwa ni 400 na ni wale waliopo kwenye orodha ya kuombwa michango, Wamiliki waleseni za uchimbaji wa kati –02, Wamiliki wa leseni za utafiti –11,Wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo, plant na wanunuzi –100,Taasisi za Serikali,mashirika–NEMC,RUWASA, OSHA, GCLA, GST, STAMI CO, Tume ya Madini , TFS, Bondela Maji la Kati ,TANROADS,Zimamoto na Uokoaj i , VPO–Mazingira, TFS, TANESCO, TARURA, SUWASA, WMA, Chamber of Mines,Wizara–Madini, Maj i na Umwagiliaji ,Uwekezaji.

Alisema wadau wengine walioalikwa ni maofisa 10 kutoka Ofisi ya mkuu wa mkoa, Maafisa Watendaji wa Kata–20,Maafisa Watendaji wa Vijiji–70, Wenyeviti wa Vijiji–20, Chama Tawala–10, Baraza la Madiwani –28,Watu maarufu na Viongozi wa dini –10,Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri –22.

Mwenda alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha watu wote walioalikwa kwenye kongamano hilo ambalo litafanyika kwenye ukumbi mkubwa wa Halmashauri ya wilaya hiyo uliopo mjini Kiomboi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com