WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent
Bashungwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala
na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule
kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki
Shemdoe,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na
mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda
hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu anayeshughulika Elimu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli, akizungumza wakati
wa uzinduzi wa kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu
wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika
leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Katibu wa
TSC Bi.Paulina Nkwama,akielezea malengo ya mkutano wakati wa uzinduzi wa
kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na
wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari
14,2022 jijini Dodoma.
Muwakilishi
wa Kamishna wa Elimu Bw.Venance Manoni, akizungumza wakati wa uzinduzi wa
kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na
wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari
14,2022 jijini Dodoma.
Baadhi ya
washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kalenda ya
utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu
wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Afisa
Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Abdul Maulid akitoa neno la shukrani kwa
niba ya washiriki kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa (hayupo pichani) mara baada ya
kuzindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa
mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari
14,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent
Bashungwa,akizindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa
elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda.Wengine Pichani ni
Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe (wa pili Kulia),Naibu Katibu Mkuu
anayeshughulika Elimu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli (Kushoto).Muwakilishi wa
Kamishna wa Elimu Venance Manoni (wa Kwanza Kulia) hafla ya uzinduzi huo
umefanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa akisoma maandishi baada ya kuzindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda hafla iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa akiwa katika picha mbalimbali za pamoja na washiriki mara baada ya kuzindua kalenda ya utekelezaji wa mitaala na mafunzo kwa maafisa elimu wa mikoa na wathibiti wakuu wa ubora wa shule kanda iliyofanyika leo Januari 14,2022 jijini Dodoma.
Na Alex
Sonna, Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa ametoa maelekezo saba kwa
viongozi wa Mikoa na Halmashauri ikiwemo kuhakikisha hakuna
mwanafunzi wa elimu ya awali, darasa la kwanza au kidato cha kwanza anayetozwa
mchango wowote kama sharti la mwanafunzi kuandikishwa.
Maagizo hayo ameyatoa leo Januari 14,2022
Jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo kwa Maafisa Elimu Mikoa, Maafisa Taaluma
Mikoa na wathibiti ubora wa shule kanda pamoja na kuzindua kalenda
za utekelezaji wa Mitaala ya elimu ya Awali,Msingi na Sekondari.
Waziri Bashungwa amesema wakati shule za
msingi na sekondari zinatarajiwa kufunguliwa tarehe 17 Januari, 2022, kumeanza
kutokea malalamiko toka kwa wananchi, kuhusu kutozwa michango mbalimbali, bila
kufuata utaratibu.
“Wanafunzi kupelekwa kuandikishwa shule, na
kisha kuambiwa shule zimejaa, au wazazi kuwapeleka shule wanafunzi, na kukuta
shule haina mwalimu anayetakiwa kuwandikisha shule, kwa maana wanakuta shule
zimefungwa,”amesema.
Amesema changamoto hizi, zimekuwa zikileta
usumbufu kwa wazazi na wanafunzi pamoja na kuleta usumbufu usio wa lazima kwa
wananchi.
Amesema vikwazo na kero hizi zimefifisha kwa
kiasi kikubwa, uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na elimu ya awali.
Kutokana na hali hiyo Waziri Bashungwa
amewaelekeza viongozi wa Mikoa, Halmashauri na Shule, kuhakikisha
hakuna mwanafunzi wa elimu ya awali, darasa la kwanza au kidato cha kwanza
anayetozwa mchango wowote kama sharti la mwanafunzi kuandikishwa.
Pia,kila shule kuwepo na mwalimu mmoja kwa
ajili a kuandikisha watoto katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wapo likizo.
“Viongozi wote wa Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa, kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa Mwongozo wa utoaji wa
Elimumsingi Bila Malipo. Mheshimiwa Rais ameongeza fedha zinazotolewa kila
mwezi, kwa ajili ya kugharimia elimu bila malipo, kutoka shilingi bilioni 23
kwa mwezi hadi kufikia bilioni 26 kwa mwezi,”amesema.
Pia amewaelekeza Maafisa elimu wa kata kwa
kushirikiana na watendaji wa kata,mitaa na vijiji, wabainishe watoto wote
wanaotakiwa kuandikishwa shule na wawasisitize wazazi/walezi kufanya hivyo.
“Viongozi wote wa Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa kuendelea kufafanua utekelezaji wa Waraka wa Elimumsingi Bila Malipo
kwa wazazi, jamii na wanafunzi,”amesema.
Pia,kila kundi litimize wajibu wake ili
watoto wote waandikishwe, na kuendelea na masomo, katika ngazi husika.
“Kufanya zoezi la utambuzi wa watoto wenye
mahitaji maalum ni suala endelevu hapa nchini. Mwaka 2018 na 2021 Ofisi ya Rais
– TAMISEMI ilifanya ubainishaji wa watoto hao, nakuwaandikisha shule,”amesema.
Waziri Bashungwa pia ameelekeza Mikoa yote
iimarishe na kutumia vituo vya Uchunguzi Education Service Resource Assessment
Centre (ESRAC) ili visaidie katika kubainisha wanafunzi wenye mahitaji maalum,
na kushauri wapelekwe katika shule maalumu, vitengo vya elimu maalum au shule
jumuishi.
Kuhusiana na kalenda,Waziri Bashungwa
amesema kusudi la kuandaa kalenda ni kuhakikisha kuwa,
kunakuwepo na ulinganifu na usawa, wa ukamilishaji katika utekelezaji wa
mitaala wa ngazi husika, katika maeneo yote ya nchini.
“Kalenda hii ni ya kwanza
kuandaliwa na Serikali. Kalenda hii itawezesha wasimamizi wa elimu kufanya
usimamizi, ufuatiliaji, na tathmini ya utekelezaji wa mitaala kwa urahisi,”amesema
Vilevile, kalenda hiyo itawapa fursa
wanafunzi wanaohama kutoka shule moja kwenda nyingine kuwa na mwendelezo wa
aina moja wa mada zinazofundishwa.
Waziri Bashungwa
amewaagiza Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya, kuwasimamia
Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu wa Masomo, kuzingatia kalenda ya
utekelezaji wa mtaala, ili wawe na ufundishaji na ujifunzaji wenye tija na
mahiri, badala ya kuwekamsisitizo katika ukaririshaji wa mada.
“Hivyo, natumia fursa hii kuwaagiza Maafisa Elimu Mikoa, kutoa mafunzo ya matumizi ya Kalenda ya Utekelezaji, katika Halmashauri zenu zote, kabla au ifikapo tarehe 1 Februari, 2022,”amesema.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment