Mkuu wa wilaya ya singida Mhandisi Paskasi Muragili akiwa na Mkurugenzi wa Trees for the future Heri Rashidi akipanda mche wa mti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upadaji miti katika kijiji cha Munkhola jana.
Baadhi ya wananchi wakishiriki zoezi la upandaji miti wakati wa uzinduzi .
Baadhi ya wafanyakazi na maafisa kutoka shirika la trees for furure wakipunga mikono kwa wanachi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti .
WANANCHI waliovamia hifadhi ya msitu wa Mukhola uliopo kata ya mgori katika halmashauri
ya singida wametakiwa kuondoka kwenye hifadhi hiyo vinginevyo watakamatwa na
kuwekwa ndani
kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti amabyo imeratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Trees for future Mkuu wa Wilaya ya Singida mkuu wa wilaya ya singida Mhandisi Paskas Muragali ameagiza kukamatwa kwa Wananchi Wanaovamia Hifadhi hiyo kwa kuharibu mazingira na kupelekea kukosekana kwa mvua .
"Tumekuwa kwa sehemu kubwa sana tukiaribu mazingira yetu lakini pia tumekuwa wa kwanza kulalamika hatupati mvua yakutosha , hapa kwenye msitu huu wa munkhola kuna watu wameenda kule juu wanakata miti wanalima na nimepata taarifa . naomba kuagiza kuwa wale wote waliolima msimu wakamatwe na sheria ifate mkondo wake" . alisema Dc Muragili.
Mwenyekiti wa halamshauri ya singida Elia Digha amesema wao kama viongozi hatakuwa tayari kushuhudia misitu ya mkoa wa singida ikifyekwa na kusema kuwa hata kiongozi yeyote atakayehusika na uharibifu huo atawajibishwa kwa mijibu wa sheria.
" Tusiruhusu eneo hili aina yeyeote ya mtembea kwa miguu , mshika shoka au fimbo wa kuaharibu msitu , naomba mkuu usimamie imara kuhakikisha msitu unasalimika haijalishi ni nani na kama ni kiongozi anajihusisha na hili awajibishwe". alisema Mwenyekiti huyo.
Mkurugenzi wa shirika la tree for future Heri Rashid akiwa kwenye uzinduzi huo wa kampeni ya upandaji miti ndani ya halmashauri ya singida amesema kwa sasa wamshirikiana na halmashauri hiyo kuwajengea uwezo wananchi kupanda miti ili kuboresha mazingira yao ambayo yamekuwa si salama kwa kukosa hewa nzuri.
" Mzingira yameharibiwa sana kwa shughuli za mbalimbali za binadamu kwa kukata miti kulima na mambo mbalimbali sasa mwaka huu tunashirikiana na halmshauri ya singida kama juhudi zetu za kuhamashisha wananchi kupanda miti kwa wingi ili kurudishia uoto wa asili uliopotea. " alisema Mkurugenzi wa Trees For The Future Heri Rashid alipozungumza na waandishi wa habari.
Licha ya tishio hilo la
kukamatwa kwa wale waliovamia hifadhi hiyo baadhi ya wakazi wa vijiji jirani hifadhi hiyo wamesikitishwa na uamuzi
huo wa kuwaondoa katika maeneo hayo wakidai kuwa ni ya kwao tangu zamani.
"Tunashangaa watu sahivi wamepanda hadi kwenye mashamba yetu watu tayari wameshalima tumeona sisi hatuna haki kwenye tanzania hiii . Tulishangaa mnaambiwa shukeni mpande miti na sisi hatukuwa na taarifa ya aina yeyote wanankijiji wanalalamika kwa sababu walikatiwa eneo hili na serikali" . Walisema baadhi ya wananchi wakilalamikia uamuzi huo.
Kwa mkoa wa singida Shirika
la trees for future kwa kushirikiana na halmashauri ya singida, iramba, ikungi na
mkalama kuijengea uwezo juu ya elimu ya utunzaji wa mazingira na
kuwaongezea usalama wa chakula kupitia kilimo.
0 comments:
Post a Comment