METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, January 6, 2022

TAFITI ZINAONESHA WACHIMBAJI MADINI WENGI HAPA NCHINI NI WANAUME-WAZIRI DKT. BITEKO

Tafiti zinaonesha kuwa, uchimbaji wa madini kwa miaka mingi umekuwa ukifanywa na wanaume kuliko wanawake  ambapo kati ya wachimbaji wadogo wa madini 100, wanawake ni 7 peke yake.

Hayo ameyasema Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko alipotembelea mgodi wa uliopo katika kijiji cha kata ya wilayani Gairo mkoa wa Morogoro.

Huko nyuma wachimbaji wadogo wote nchini walikuwa wanachangia chini ya asilimia 4 kwenye pato la madini lakini sasa hivi wachimbaji wadogo wanachangia zaidi ya asilimia 30 kwenye pato la madini.

Kwa hatua hiyo, Sekta ya Madini inauhakika wa kufikia asilimia 10 ya mchango wake kwenye pato la taifa ifikapo mwaka 2025.

Sambamba na hayo, Dkt. Biteko amesema Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeingia mkataba na Benki mbalimbali nchini ili kuwadhamini wachimbaji wadogo waweze kukopesheka ili wachimbe kwa tija.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabiri Makame amempongeza Dkt. Biteko kwa kufanya ziara wilayani Gairo ambapo amesema ujio wa Waziri wa Madini unaenda kuzimaliza changamoto zinazo wakabili wadau wa madini wilayani humo.

"Tunaomba utufikishie salamu zetu kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea maendeleo katika Wilaya yetu ya Gairo, mwambie tunamshukuru sana," amesema Dkt. Biteko
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com