Mkuu wa mkoa wa singida Dkt. Binilith Mahenga akizungumza na wajumbe wa kamati ya mradi wa korosho wilaya ya manyoni akiwa ameambatana na Bi Rahabu Mwagisa mkuu wa wilaya ya manyoni alieko kulia na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya manyoni Melkzedeki Humbe .
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya mradi wa korosho wakiwa katika kikao na mkuu wa mkoa wa singida , kushoto ni fadhil chimsala afisa kilimo wilaya ya manyoni.
Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Aderaide Rweikiza akitoa taarifa mradi wa kilimo cha korosho na Hali halisi ya ugawaji wa mashamba ya korosho kwa watu waliolipia fedha .
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akitoa maelekezo ya namna ya kutatua mgogoro utokanao na mashamba ya korosho ambapo imedaiwa kuwa zaidi y ash. Milioni 600 zimetoka kwa watu kwaajili ya kununua mashamba hayo.
Na Hamis Hussein - SINGIDA
KAMATI ya mradi
wa kilimo cha korosho kutoka halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani hapa
imetakiwa kutoa taarifa ya kina kufuatia madai ya kupokea zaidi ya Sh.milioni 600 kutoka kwa
watu 180 kutoka ndani na nje ya nchi
ambao waliahidiwa kuwapatia mashamba ya kulima korosho lakini hawajagawiwa
maeneo hayo ikiwa ni miaka minne sasa.
Kufuatia malalamiko ya watu waliotoa fedha hizo kwa kuziweka
kwenye akaunti maalumu ya halmashauri kama walivyokuwa wameelekezwa, Mkuu wa
Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge aliitisha kikao cha kamati tendaji ya
mradi wa korosho Manyoni na amesema amepokea orodha ya watu 180 kutoka ndani na
nje ya nchi wakilalamikia kutopata mashamba hayo na pesa tayari walishatoa.
Kikao hicho kilicho wakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo
wale wa kilimo , wataalamu kutoka idara mbalimbali, viongozi wa halmashauri ya
manyoni , mkuu wa wilaya hiyo Bi. Rahabu
Mwagisa pamoja na mkuu wa mkoa wa singida Dkt. Binilith Mahenge kililenga
kutafuta suluhu ya mgogoro huo wa mashamba ya korosho ambao umekuwa kwa muda
sasa na kupitia kikao hicho ,Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa aligiza
kufungwa akaunti zote za kupokea fedha za ununuzi wa mashamba hayo hadi
utakapofanyika uhakiki wa kujiridhisha.
Sanjari na hilo Mkuu wa Mkoa Dk.Mahenge aliiagiza kamati hiyo
hadi kufika Jumatatu ya Januari 17 mwaka huu iwe imetoa taarifa ya mradi huo
iliyosahihi ambayo itapitiwa na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) Mwalimu Doroth
Mwaluko kabla ya kuwasilishwa katika
ofisi ya mkuu wa mkoa.
Kando ya agizo hilo pia Dkt.Mahenge aliwataka kuandaa upya na
kufuatia taarifa iliyokuwa ikitolewa
kutojitosheleza kwani majina ya baadhi ya watu wanaodaiwa kulipia fedha
hayakuwepo licha ya yeye kuwa nayo huku kiasi cha fedha kilichopokelewa kikiwa
hakijabainishwa.
"Taarifa
hiyo muiandae vizuri najua hizo namba mnazo nendeni mkaziunganishe na muwe
makini kama kuna watu walikuwa wakiingiza fedha hizo benki mnapaswa kuwajua,
wapo walioleta fedha hizo ofisini, mliowapa mashamba, ambao bado hamjawapa,
waliopanda au kupalilia hivyo nawaombeni tengenezeni taarifa inayojitosheleza," alisema Dkt.
Mahenge.
Mkuu huyo wa mkoa wa singida mwenye uzoefu mkubwa wa utendaji
serikalini aliostajabishwa namna kamati
hiyo ilivyokea fedha za watu kwaajili ya mashamba hayo na watendaji wake wasiwe
na taarifa sahihi.
"Haiwezekani mkapokea fedha za mtu halafu mkashindwa kuandaa taarifa kwani jambo
hilo sio geni kwao na kama taarifa hiyo inashindwa kuandaliwa vizuri patakuwa
na kizungumkuti hamna taarifa hizo huenda zitakuwa kwa mtu mmoja bila
kushirikishwa wengine na hawajui lakini kama wajumbe wote wa kamati hiyo
wangekuwa wanajua isingeshindwa kuandaliwa” Alisema Dkt. Mahenge katika kikao hicho .
Licha ya kutoa agizo kwa kamati ya korosho mkoa wa singida
hususani katika halmashauri ya Manyoni Dkt. alitaka changamoto hiyo waimalize
na kuwa jambo hilo anamuachia mkurugenzi na lifanyike chini ya Katibu Tawala na
sio kuiachia kamati hiyo peke yao na kuwa kama watashindwa kupata mzani waende
kwenye hayo mashamba kujiridhisha kwa kuhakiki majina ya wamiliki wa mashamba
hayo.
Alisema taarifa mpya
watakayoitoa baada ya kuipitia kwa makini inapaswa ioneshe fedha zilizopokelewa na mashamba yake huku akionesha wasiwasi kuwa kuna uwezekano wa fedha zilizoingizwa zikawa
ni zaidi ya ekari za mashamba walizonazo
hivyo waeleze kuwa kutokana na kutofunga akaunti walipokea fedha hizo ili kama
kutakuwa na uwezekano watu hao ambao watakosa maeneo watafutiwe sehemu nyingi
kama Itigi au Ikungi kwa makubaliano kwa sababu shida yao ni kupata mashamba.
Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Manyoni ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo Aderaide Rweikiza alisema mradi huo wa korosho mkoani singida ulikuwa ni matokeo ya andiko lilikuwa limeanisha miradi mbalimbali ya maendeleo na kupitia andiko hilo liliambana na utafiti kuwa wilaya ya manyoni ndio inaweza kuzalisha korosho kwa mkoa wa singida hivyo mchakato ukaanza mwaka 2017 kwa kuwashirikisha wakulima kwa kuwagawia ardhi kwa bei elekezi.
“Ulipendekezwa
mradi wa korosho ukaoneka kuwa unaweza kulimwa manyoni , mheshimiwa mkuu wa
mkoa mwaka 2016 tulipeleka andiko letu
lakini tukaona kwamba andiko bado halija kamilika tukaona tusiombe mkopo , tukaona tukalibishe wakulima
ambapo wanaweza kuwa kwenye mradi wetu na tukaona wakulima wachangie” alisema
mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya manyoni .
0 comments:
Post a Comment