METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, December 26, 2021

Waziri Bashungwa Ampiga Tafu Mbunge Mtaturu//Ashauri Mazito Kilele Cha Mtaturu Cup 2021 Ikungi-Singida

 
















Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewataka madiwani kuipa kipaumbele zaidi ajenda ya ujenzi na uboreshaji wa miundo mbinu ya viwanja vya michezo katika halimashauri zao, akisistiza kuwa michezo ni kipaumbele kikubwa kwa jamii, kama ilivyo kwa vipaumbele vingine.

Waziri Bashungwa ametoa wito huo Desemba 26, wakati akizungumza katika fainali ya ligi ya Mtaturu Cup iliyofanyika viwanja vya shule ya Sekondari Ikungi mkoani Singida.

Amesema Serikali inatamani kuboresha viwanja vyote vya michezo ili viwe na viwango vinavyostahili lakini wakati mchakato ukiendelea ndani ya Serikali ni vyema madiwani kupitia vikao vyao vya  halimashauri wakaipa kipaumbele ajenda ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya viwanja vya michezo katika maeneo yao.

Kauli ya waziri Bashungwa inafuatia risala ya kamati ya uratibu wa ligi hiyo kudai kuwa, wanakabiliwa na miundombinu duni ya viwanja vya mchezo wa soka pamoja na uelewa hafifu wa sheria zinazo utawala mchezo huo.

Kuhusu uelewa mdogo wa sheria za mchezo wa Soka, Waziri Bashungwa amewahahidi wakazi wa Ikungi kuwa,  atawaagiza wataalam kutoka Chuo cha Michezo cha Malya kufika wilayani Ikungi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya masuala mbalimbali yanayo tawala mchezo huo.

Awali akizungumza katika kilele cha Mtaturu Cup mwandaaji wa ligi hiyo ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ikungi, Mhe. Miraji Mtaturu amesema dhamira kuu ya mashindano hayo imefikiwa kwa kiwango kikubwa, na kuhahidi kuwa ligi hiyo itakuwa endelevu kwa lengo la kujenga mshikamano zaidi kwa vijana.

Naye Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Jerry Muro ameitumia fursa hiyo kuelezea furaha yake akisema  uwepo wa ligi ya Mtaturu Cup umeongeza mwamko wa vijana kushiriki katika michezo na kukuza uhusiano, kutokana na ukweli kuwa michezo ya aina hiyo ni starehe iliyokosekana kwa muda mrefu katika jimbo hilo.

Ligi ya Mtaturu Cup imeusisha zaidi ya michezo ya 40 ambapo imewezesha jumla ya vijana 30 kuchaguliwa maalum kwa ajili ya kuunda timu ya wilaya itakayokuwa ikishiriki ligi na mashindano mbalimbali kwa ngazi ya mkoa na taifa.

Katika fainali hizo timu ya  Matongo imebuka mabingwa wa ligi ya Mtaturu Cup kwa kuichapa bao mbili kwa nunge timu ya Mampando na kujizolea zawadi ya kombe pamoja na shilingi milioni moja na laki tano.


Mwisho.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com