METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, December 13, 2021

MICHEZO YA SANAA KUTIKISA TAIFA CUP 2021,KUANZA KESHO

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa CUP 2021 Yusufu Omary Singo (katikati) wakiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Ufundi ya Taifa CUP Jackson Beda (kushoto) na Leah Kihimbi (kulia) Mkurugenzi Msaidizi wa Sanaa  kwenye mkutano na waandishio wa habari kuzungumzia  Uzinduzi wa Sanaa za maonesho kwenye Taifa CUP  hapo kesho  jijini Dar es Salaam

Na. John Mapepele 

Mikoa yote ya Tanzania Zanzibar na zaidi ya mikoa kumi Tanzania Bara inashiriki michezo ya sanaa za maonesho inayoanza kesho kwenye mashindano ya Taifa CUP 2021 inayoendelea jijini Dara es Salaam hivyo kuleta vionjo vya aina yake katika mashindano ya mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo, Omary Yusufu Singo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Michezo nchini kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari leo, Disemba 13, 2021 kwenye ukumbi wa mkutano wa Uwanja wa Benjemini Mkapa jijini Dar es Salaam.

 Singo amesema mashindano ya mwaka huu ambayo yameshirikisha michezo ya Soka kwa wanaume na wanawake, netiboli na riadha yameongezewa vionjo kwa kushirikisha sanaa za maonesho ambazo zitashindanisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani  ili kuibua  vipaji katika  fani za muziki wa Singeli  na Muziki wa kizazi kipya.

Mratibu waTamasha hilo la Sanaa za maonesho, Bi Leah Kihimbi ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Sanaa nchini amesema kuwa mashindano hayo siyo tu yanaongeza radha mpya ya Taifa CUP 2021 bali yatasaidia kutoa fursa ya pekee kwa wasanii ambao watatumbuiza na kubahatika kupata nafasi za kuendelezwa.

Amesema mashindano hayo yanatarajia kuwa ya siku mbili na kuanza kesho na yatakuwa yakifanyika ukumbi wa Uwanja wa Taifa kuanzia saa moja usiku.

Ametoa wito kwa vyama na mashirikisho mbalimbali kutumia nafasi hii kuja kupata vipaji ambavyo wanaweza kuviendeleza ili kufanya vizuri zaidi kwenye ngazi za kimataifa.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Taifa CUP 2021 Jackson Ndaweka ambaye pia ni Katibu wa Shirikisho la Riadha Tanzania amesema kwa upande mchezo wa soka  wanaume tayari  timu za Mara na Mjini Magharibi zimefuzu  kuingia nusu fainali leo wakati soka wanawake timu ya Mkoa wa Dar es Salaam imekuwa timu ya kwanza kufuzu kuingia nusu fainali baada ya kuichabanga Mjini Magharibi magoli 2-1.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com