Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 01 amefanya ziara ya kukagua
miradi ya Maendeleo Wilaya ya Kinondoni ambapo akiwa katika Mradi wa
Maboresho ya Mto Ng’ombe unaogharimu Shilingi Bilioni 32 ukiwa na urefu
wa Km 7.5 amechukizwa kuona hakuna chochote kinachoendelea kwenye mradi
licha ya Viongozi wa Wilaya kumdanganya kuwa Mkandarasi yupo Site
anaendelea na kazi wakati wa kikao kazi kilichofanyika siku 6 zilizopita
kwenye ukumbi wa Karimjee.
Kutokana na hilo RC
Makonda amemuagiza Mshauri wa Mradi kumuita Mkandarasi huyo Mara moja
ofisini kwake ili aeleze nikwanini kazi haifanyiki wakati tayari mkataba
umesainiwa tokea 16/06/2019.
Aidha RC Makonda
amemuagiza mkandarasi huyo kuhakikisha kazi hiyo inakamilika na
kukabidhiwa ndani ya miezi 10 kuanzia sasa tofauti na miezi 18
waliyoomba huku akiwaonya Watendaji wanaoendelea kumpa taarifa za wongo
kuwa Yeye, Katibu tawala wa Mkoa huo na Kamanda Mambosasa wataendelea
kufanya ziara kwenye kila mradi kujionea kama taarifa wanazoletewa
kwenye karatasi zinaendana na kinachofanyika Site.
Akiwa kwenye Mradi wa
ujenzi wa Soko la Kisasa Magomeni linalogharimu kiasi cha Shilingi
bilioni 8.9, RC Makonda amemtaka mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana
ili kuhakikisha Soko hilo linakabidhiwa Mwezi Disemba mwaka huu.
Pamoja na Hayo RC
Makonda ameielekeza Manispaa ya Kinondoni kuhitisha kikao na
Wafanyabiashara wa soko hilo ili wakubaliane namna ya kuweka jografia ya
soko hilo ikiwa ni pamoja na sehemu za maduka,vizimba na eneo la
kushusha mizigo.
Pamoja na hayo RC
Makonda ametembelea mradi wa Ujenzi wa Soko la Tandale unaogharimu kiasi
Cha shilingi Bilioni 8 na kuelekeza Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha
mkandarasi anafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha anakabidhi kazi
ndani ya Miezi sita kuanzia sasa.
0 comments:
Post a Comment