METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 17, 2021

DKT.ABBASI AWAFUNDA WASANII CHIPUKIZI TAIFA CUP 2021

 

Na John Mapepele

Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amewataka Wasanii chipukizi walioshiriki Taifa CUP 2021 kuishii maisha halisi na kuzingatia  maadili ya  taaluma zao kama walivyofundishwa kwenye  mafunzo maalum ya siku tatu yaliyoandaliwa na Wizara ya Kamati ya kitaifa ya Taifa CUP 2021 katika kipindi hiki cha  mashindano.

Akizungumza leo, Disemba 16, 2021 kwenye siku ya mwisho wa semina maalum kwa washiriki wote 32 waalioshiriki kwenye onesho la Sanaa za muziki wa Singeli na kizazi kipya kwa wasanii chipukizi kutoka  mikoa yote ya Zanzibar  na kumi upande wa Tanzania Bara lililomalizika jana amesema kama  kuna kitu cha msingi kinachoweza kuwasaidia  wasanii hao chipukizi kupata mafanikio  katika  maisha yao  ni kuzingatia maadili ya taaluma zao.

“Wasanii wengi wasiozingatia maadili wanaweza kuwa maarufu lakini hawawezi kuwa na mafanikio katika maisha yao.” amefafanua Dkt. Abbasi

Kufuatia hali hiyo Dkt. Abbasi amesema Wizara yake inakwenda kuandaa Semina maalum ya maadili ya kibiashara katika muziki itakayowakutanisha wenye makampuni na wasanii ili wasanii waweze kujua matarajio ya wenye makampuni wakati wanapowatumia kwenye biashara zao.

Katika semina hiyo, Dkt. Amewafundisha siri sita za kufikia kwenye mafanikio kwa msanii ambapo amefafanua kuwa yeye ameziishi siri hizo had i alipofika sasa.

Akifundisha kwa mifano na uzoefu, Dkt. Abbasi amezita siri hizo za kufikia mafanikio kuwa ni pamoja na kuweka lengo, kuweka lengo kubwa, kuendelea kusimama kwenye malengo uliyojiwekea, kujitangaza (branding) kuzingatia maadili na kumtegemea mwenyezi Mungu kwenye kila jambo.

katika shindano la Singeli lililomalizika jana, Hamza Hamza kutoka Mkoa wa Morogoro ameibuka mfalme wa mashindano hayo wakati Abdulkadiri Kwangaya kutoka Dar amekuwa mshindi wa pili na Saleh Zuber ameibuka mshindi wa tatu.

Kwa upande wa muziki wa kizazi kipya Abisai Kassanga kutoka mkoa wa Pwani ndiye bingwa wa mwaka huu akifuatiwa na Meshack Ngemela kutoka Mbeya na nafasi ya tatu imekwenda kwa mapacha Asma na Asnath Athumani.

Baada ya fainali za mashindano hayo Dkt. Abbasi alitoa salam za pongezi kwa  washiriki wote kutoka kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan, ambapo pia alisema Wizara inatoa zawadi kwa washiriki wote kupata mafunzo yam waka mmoja.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com