METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, June 20, 2021

WAZIRI MKENDA AKABIDHI MATREKTA YA KUVUNIA KWA WAKULIMA WA MPUNGA WILAYANI MBARALI, AIPONGEZA BENKI WA WAKULIMA-TADB

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mbarali, tarehe 20 Juni 2021 wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wakulima wa Mpunga katika kijiji cha Imalilosongwe kilichopo kata ya Ubaruku wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakifuatilia hotba yaWaziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda wakati wa makabidhiano ya Zana za Kilimo zilizotolewa kwa wakulima na Benki ya Kilimo (TADB), tarehe 20 Juni 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akikabidhi mfano wa hundi ya Milioni 950 iliyotolewa na Benki ya Kilimo (TADB) kwa wakulima katika kijiji cha Imalilosongwe kilichopo kata ya Ubaruku wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, tarehe 20 Juni 2021.
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mbarali, tarehe 20 Juni 2021 wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya.
Muonekano wa Matrekta ya kuvunia yaliyotolewa na Benki ya Kilimo (TADB) na kukabidhiwa na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda kwa wakulima katika kijiji cha Imalilosongwe kilichopo kata ya Ubaruku wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, tarehe 20 Juni 2021.
Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo Tanzania (TADB) akisisitiza jambo kabla ya kumaribisha mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda kwa ajili ya kukabidhi Zana za Kilimo zilizotolewa kwa wakulima na Benki ya Kilimo (TADB) katika kijiji cha Imalilosongwe kilichopo kata ya Ubaruku wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, tarehe 20 Juni 2021.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mbeya


Katika kuchagiza mapinduzi ya Kilimo nchini Benki ya Kilimo-TADB imekabidhi zana za kisasa za kilimo kwa wakulima 15 kutoka ushirika wa nguvu kazi Mwanavala ikiwa ni sehemu ya kutekeleza lengo kuu la uanzishwaji wake.


Katika kufikia mapinduzi ya kilimo nchini serikali imeweka sera na mikakati mbalimbali itakayowezesha nchi kufikia mapinduzi hayo makubwa ikiwa ni pamoja na mkakati wa zana za kilimo wa mwaka 2006 ambao ulikuwa chini ya mpango wa maendeleo ya kilimo awamu ya kwanza (ASDP I) lakini pia mpango wa maendeleo ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).

 

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 20 Juni 2021 wakati akizungumza na wakulima wa Mpunga katika kijiji cha Imalilosongwe kilichopo kata ya Ubaruku wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.


Waziri Mkenda ameipongeza Benki ya Kilimo-TADB kwa kuidhinisha mkopo wenye thamani ya Tsh Milioni 949 ambao umewezesha upatikanaji wa zana za kisasa za kuvunia kwa wakulima 15 katika kata ya Imalilosongwe wilaya ya Mbarali.


Pamoja na kukabidhi zana hizo kwa wakulima hao Waziri Mkenda amesema kuwa zana hizo zitakuwa sehemu ya kuimarisha ufanisi wa kazi na sehemu ya kupunguza upotevu wa mazao kwa kiwango kikubwa zaidi nchini ambao unatajwa kuwa kati ya asilimia 15 hadi 40.


Matrekta hayo yaliyokabidhiwa na Waziri Mkenda ni sehemu ya matrekta 15 ya kuvunia kwa wakulima wilayani Mbarali ambapo miongoni mwao waliokabidhiwa zana hizo za kilimo ni vijana watatu wa kike.


Waziri Mkenda ameipongeza Benki ya TADB kwa kuona umuhimu wa kuwakopesha wakulima zana hizo bora huku akionyesha kupendezwa na utoaji huo wa mikopo kwa wakulima wanawake.


Waziri Mkenda amewataka wakulima hao kuhakikisha kuwa wanatumia ipasavyo mashine hizo pamoja na kuzitunza vizuri ili kuimarisha uyendaji kazi wao katika kilimo.


"Nitoe wito kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali na vyombo husika vya ulinzi na usalama, naomba mshirikiane kwa pamoja na wananchi hawa ili kulinda mashine hizi na kuepusha hujuma za aina yeyote kwa mashine hizi kwa wakulima hawa" Amekaririwa Mhe Mkenda na kuongeza kuwa


"Mashine hizi zimenunuliwa gharama kubwa hivyo ni muhimu pia kuvitunza na kuvilinda kwa ukaribu ili viweze kudumu na kutuletea matokeo ambayo tunayoyatarajia"


Akitoa taarifa ya mikopo iliyotolewa na Benki ya Kilimo Tanzania-TADB Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Ndg Japhet Justine amesema kuwa hadi sasa TADB imetoa jumla ya Bilioni 300 katika minyororo ya thamani ya mazao mbalimbali kama vile mahindi, kahawa, pamba, mbogamboga, alizeti na matunda pia katika sekta ya mifugo na uvuvi ambayo imewanufaisha wakulima milioni 1.8 nchi nzima.


Amesema kuwa pamoja na mikopo ya moja kwa moja, TADB kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo wadogo (SCGS) imekwisha idhinisha mikopo yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.4 kwa wakulima 4,439 katika kanda ya nyanda za juu kusini.


MWISHO

Share:

2 comments:

  1. Nauliza bank hyo unaweza kutoa mkopo kwa familia au mtu mmoja mmoja kwajili ya biashara ya kikimo? 0768536091

    ReplyDelete

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com