METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, November 5, 2021

WAZIRI BITEKO AWEKA WAZI MAFANIKIO YA SERIKALI KATIKA SEKTA YA MADINI TANGU UHURU

Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko,akizungumza na waandishi wa habari  leo November 5,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya wizara yake  kuhusu mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru.

Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko,akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo November 5,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya wizara yake  kuhusu mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya wizara yake  kuhusu mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru leo November 5,2021 jijini Dodoma

Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari  leo November 5,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya wizara yake  kuhusu mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru.

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Madini,Doto Biteko amesema ndani ya miaka 60 ya uhuru sekta ya madini imepata mafanikio makubwa ambapo madini  Tanzanite  yameongeza mapato ya Serikali kutoka shilingi milioni 166 kwa mwaka kabla ya kuwepo kwa ukuta hadi kufikia shilingi bilioni 3.9 baada ya ujenzi wa ukuta.

Pia,amesema hadi kufikia Septemba 2021 leseni hai ambazo zimetolewa za utafutaji wa madini ni 1,044 leseni 15 ni za wachimbaji wakubwa leseni 161 ni za wachimbaji wa kati na 34,000 za uchimbaji mdogo na leseni 1561 za biashara ya madini.

Akizungumza leo Novemba 5,2021 na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma,wakati akieleza mafanikio na maendeleo ya sekta ya madini kabla na baada ya uhuru,Waziri Biteko amesema sekta ya madini ina historia ndefu  kuanzia kipindi cha kabla ya uhuru hadi kufikia kipindi cha maadhimisho ya miaka 60.

Waziri Biteko amesema kuwa madini ya  Tanzanite  yameongeza mapato ya Serikali kutoka shilingi milioni 166 kwa mwaka kabla ya kuwepo kwa ukuta hadi kufikia shilingi bilioni 3.9 baada ya ujenzi wa ukuta.

“Yapo mambo mengi ambayo tumefanikiwa ikiwemo kupandisha uchumi wetu  kuongeza ufanisi wa sekta kuongeza uwazi na ushiriki wa watanzania,”amesema.

UTOROSHWAJI WA MADINI

Waziri Biteko amesema mafanikio ambayo wameyapata ni pamoja na kuzuia utoroshwaji wa madini nje ya Nchi ambapo amedai kwa sasa wamejitahidi kuweka masoko kila eneo hapa nchini.

Amesema kuwa na wasiwasi na mashaka katika utoroshaji wa madini ni jambo muhimu  haswa kwa mtu mwenye akili timamu huku akitolea mfano hata katika ndoa wasiwasi nimuhimu.

“Ni muhimu tuwe na wasiwasi siku tukiridhika kwamba mambo yapo swari ujue siku hiyo ndio tumeanza kuibiwa kuwa na wasiwasi na mashaka kwa mtu mwenye akili timamu ni bora lakini twende kwenye namba.

“Turudi nyuma tulipotoka ni kesi za watu wangapi walikuwa wakikamatwa? wakitorosha madini, wachimbaji na wafanyabiashara ukikuatana nao watakwambia kutorosha kuna hasara zamani walikuwa wanatorosha kwa sababu hapa ndani hapakuwa na utaratibu mzuri.

“Tuendelee kuwa na wasiwasi kwa sababu kuwa na wasiwasi ni sehemu ya maisha muhimu mtu akisema atatorosha tujue uchochoro.

“Niwape wito watanzania kutorosha madini ni zilipendwa hakuna faida hakuna tija mtu yeyote anaetorosha madini kama tulivyosema anatafuta vitu viwili tu kwenye maisha yake anatafuta jela ama umaskini na wachimbaji wetu hawahangaiki na kwenda jela.

AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUTOA VIBALI VYA AJIRA

Waziri Biteko amezitaja baadhi ya  changamoto ambazo Wizara imekutana nazo katika kipindi cha miaka 60  ni pamoja na matokeo ya maendeleo ambapo kwa sasa rasilimali fedha,vitu na watu zinahitajika.

“Changamoto kubwa kwetu ni matokeo ya maendeleo kama ambavyo kwenye maisha ya kawaida tu ukifanikiwa jambo moja utazalisha jambo lingine,kwa mfano sekta inapokuwa inavutia watu wengi kuingia katika sekta kwahiyo upande wa pili inavutia watu wengi na rasilimali zenyewe ni fedha,vitu na watu,”amesema.

Hata hivyo,Waziri huyo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiri watumishi wapya  ambapo amedai itapunguza changamoto ya uhaba wa watumishi.

Ameitaja changamoto nyingine ni utengenezaji wa sheria zinazofanana  ambapo amesema ni lazima   Waafrika wawe na sheria zinazofanana ili kuendelea kulinda rasilimali madini katika maeneo yao.

“Mfumo wa usimamizi wa madini sisi Tanzania hatupo peke yetu tuna majirani zetu ambao wana madini kama sisi hivyo ni lazima sasa changamoto ninayoiona ni ya kiafrika zaidi Ni lazima waafrika tusimame tuwe tunasheria zinazofanana,”amesema.

Vilevile,amesema changamoto nyingine ni mtazamo wa wachimbaji wadogo kuvamia waeneo ya wawekezaji ambapo amedai Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuwalinda wawekezaji wenye leseni.

“Mwekezaji lazima alindwe ni muhimu watanzania tuwalinde wawekezaji wetu haina maana tunampa mtu leseni halafu anaingiliwa katika biashara zake.

WATAALAMU WAPO TENA WA KUTOSHA

Katika hatua nyingine,Waziri Biteko amesema kwa sasa watanzania wapo tayari kuchimba madini kwani kuna watalamu wengi na wa kutosha tofauti na miaka ya nyuma ambayo Hayati Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere alidai mpaka watanzania wawe tayari ndio wachimbe madini.

“Tumejaribu kuonesha hata tofauti ya wakati wa wakoloni na sisi  tumepiga hatua kubwa sana na utayari wetu ni kuwa na wataalamu wa kusimamia madini.Nchi hii inazalisha Wajiolojia,Wahandisi wengi sana migodi yetu unayoiona hata wachimbaji wadogo asilimia zaidi ya 80 wana Wajiolojia wao.

“Kwa hiyo kile ambacho baba wa Taifa alisema tukiwa tayari tuchimbe madini yetu mimi naamini wakati ndio huu tupo tayari kwa sababu tuna watalaamu,”amesema.

UWAZI WA MIKATABA

Aidha,Waziri huyo amesema mikataba yote inayoingia Wizara yake haijifungii inaifanya kwa uwazi na inasaini hadharani mbele ya Waandishi wa Habari.

“Mikataba yote tunaingia Waziri hajifungii ndani akaingia mikataba na mwekezaji tunasaini hadharani na ninyi mnakuwepo(waandishi) na mikataba inawekwa hadharani.

“Isipokuwa lazima kwenye mikataba  wawekezaji wanamikataba yao ambayo hawataki ijulikane kama Nchi zipo taratibu za kufuatwa,”amesema.

MASOKO  

Kwa upande wa Masoko ya madini,Waziri Biteko amesema ndani ya miaka 60 kumekuwa na masoko mengi ya madini ambapo amedai  yamesaidia kuongeza mapato na  kwa sasa kuna masoko 50 na 52 ni madogo madogo.

“Dar tulikuwa na watu wana viwanda feki lakini vitafute kwa sasa kama vipo kwa sababu tumebadilika na hela unaipata hapo hapo na siku hiyo hiyo na mabenki yapo na tunawauliza mnataka mpewe Cash au kwa njia ya benki

“Wachimbaji wadogo wananufaika sana nenda katika Mahakama ilikuwa ni kudhulumina lakini kwa sasa hakuna kwenye masoko watu wenye hela ndio wananunua,amesema.

MAKINIKIA

Kuhusu makinikia amewahakikishia watanzania kwamba wana chaji kila aina ya madini tofauti na zamani ambapo walikuwa wakichaji katika madini ya dhahabu na almasi.

“Niwahakikishie sasa hivi kwenye makinikia haya mnayoona yanayozalishwa tunachaji kila aina ya madini yaliyopo  huku tulikotoka tulikuwa tunachaji dhahabu na almasi lakini sasa hivi tunachaji mpaka Iron iliyopo ni kiasi gani na inauzito kiasi gani,”amesema.

Amesema mara baada ya kukubaliana kutosafirisha nje ya Nchi kwa sasa wanayachukua na kuyapeleka katika maabara zao tatu ambapo zinapimwa na kuonesha kuna madini kiasi gani.

“Kwahiyo tulikubalina tubadilishe utaratibu mwaka 2020 tulisaini mkataba na ule utaratibu wa kusafirisha makinikia tunaachana  na yauzwe kama madini.Hivyo tunachukua tunapeleka kwenye maabara zetu tatu zinapima na tunalinganisha makinikia haya yana madini gani.

Amesema kutoka mwaka 2020 walivyosaini  mkataba mpaka kufika Marchi 2021 kulikuwa kuna makontena 1600 ambayo tayari yalikuwa yameishauzwa.

“Na mchango wa makinikia yenyewe katika mapato yake yote kwenye zile fedha bilioni 584 asilimia 2.5  inatokana na mauzo ya makinikia”amesema.

MIGODI

Amesema ikilinganishwa na Nchi ilipotoka hivi sasa Taifa lina migodi 9( 6 ya dhahabu,mmoja almasi,tanzanite mmoja,na mmoja wa Makaa yam awe) ambapo amedai ipo migodi takribani ya 28 ya uchimbaji wa kati na mingine mingi ya uchimbaji mdogo

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com