METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, November 6, 2021

RAIS DK.MWINYI AWAHUTUBIA WANANCHI KUADHIMISHA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WAKE ZANZIBAR

       

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Zanzibar katika mkutano wake wa kuadhimisha Mwaka mmoja wa Uongozi wake, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Zanzibar.

WANANCHI wakimshangilia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akiwahutubia Wananchi katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Uongozi wake.

  

WANANCHI na Wageni waalikwa wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayuypo pichani) akihutubia katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tuliup Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaniu Karume Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto kwake) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kulia kwake) Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dkt.Amani Karume, alipowasili katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuwahutubia Wananchi katika hafla ya kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Uongizi wake.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, alipowasili katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuwahutubia Wananchi katika hafla ya kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Uongizi wake.(Picha na Ikulu)

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com