METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, November 18, 2021

CHIFU SINGU MISSANGA ASIMIKWA KUWA KIONGOZI WA KABILA LA WANYATURU








Na Chifu Ahmed Missanga Senge

Leo Tarehe 17.11.221 imekuwa baraka Ihanja wilayani Ikungi katika Mkoa wa Singida kusimikwa ramsi Chifu Singu Missanga Senge Kuwa kiongozi wa Utemi wa UNYIKUNGU katika kabila la Wanyanturu. Hafla ya usimikwaji zilianza kwa Dua maalum ilioyo ongozwa na viongozi mbalimbali wa dini   Shekhe , Mchungaji kisha  Dua ya kimila ya Wanyaturu. Chifu Singu Missanga  amesimikwa na baraza la wazee la ukoo wa Chifu Missanga Senge katika kabila la Wanyaturu na kushuhudiwa na Chifu mkuu wa Ikungi Abraham Gwau.

Akimwakilisha Jerry Muro Mkuu wa wilaya wa Ikungi, Katibu Tawala Wilaya Ndg. Dijovison J. Ntangeki amesisitiza Viongozi wa Kimila kuwa ndio nguzo ya Amani na uwajibikaji hivyo watumie nafasi hizo kusaidia kuelelimisha jamii kuacha Mila potofu, kuhamasisha  jamii kuenzi mila na tamaduni za Tanzania. Ikiwemo uhamasishaji  upendo, maridhiano, umoja na mshikamano wa taifa ikienda sambamba na kulingania tunu za taifa pamoja na upendo ili kuondoa ukiukwaji wa Hali za binadamu wenye vionjo vya ubaguzi  pia utunzaji wa  mazingira ya asili, upandaji miti kwa wingi,kuhamasisha shughuli, za maendeleo , kilimo , ufugaji na uchapa kazi

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo Ni  Afisa Tarafa wa kijiji cha Ihanja , Mhe. Madiwani, wenyeviti serikali ya vijiji na watendaji wa kata zote . 


 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com