METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, October 1, 2021

TARAFA YA MIHAMBWE WAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA CHANJO CORONA




 Na Mwandishi wetu Mihambwe.

Wakazi Tarafa ya Mihambwe wamehasika  vilivyo kwa hiyari yao kupata chanjo ya Uviko 19 (Corona) mara baada ya kuelimishwa na huduma kusogezwa jirani na Wananchi.

"Nashukuru sana kupata chanjo ya Corona, niwaombe Watanzania wenzangu tuendane na  Dunia ilivyo, na sidhani kuna Mtanzania ama kiongozi yeyote yule anataka kuwatesa Wananchi. Tuchanje ili kupunguza madhara ya ugonjwa huu." amesema Ndaile Abdallah Ulaya mkazi Kijiji cha Dinyeke

Muuguzi Asha Kasembe amewahimiza akina Mama na Wananchi wote wapate chanjo kwani ni salama na inaimalisha kinga za mwili na kupunguza vifo na  inapunguza makali.

Pia Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ameungana na Rais Samia kupambana na ugonjwa huu kwa kuwapa elimu Wananchi, kuwahamasisha na wanaoridhia wanapata chanjo bure.

"Dunia ipo kwenye mapambano ya Uviko 19 nasi Tarafa ya Mihambwe tunaungana na Rais Samia kupambana na ugonjwa huu kwenye vijiji na vitongoji kuwaelimisha, kuwahamasisha na tumeona Watu wengi wamejitokeza kwa hiyari yao kupata kinga kutokana na huduma ya chanjo kuwafikia jirani nao. Nazidi kusisitiza Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe tuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa huu wa Corona kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa vitakasa mikono, kuepuka mikusanyiko na kupata chanjo ya sindano ya Corona" alisisitiza Gavana Shilatu.

Katika zoezi hilo Mamia ya Wananchi wamejitokeza kupata chanjo ya Corona na zoezi hilo litakuwa endelevu ndani ya Tarafa ya Mihambwe.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com