METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 9, 2021

DKT. ABBASI: SERIKALI YA RAIS SAMIA INA JAMBO NA MICHEZO

Katibu Mkuu wa Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akiwavisha medali washindi wa riadha kwenye fainali za Mashindano ya Riadha ya Taifa jijini Arusha leo Oktoba 9, 2021 

Katibu Mkuu wa Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi (mwenye miwani) akiwa na viongozi mbalimbali wa michezo nchini, nyuma ni washindi wa riadha katika mashindano hayo 

Wanariadha wa mbio za mita 10000 kwa wavulana wakishindana   leo Oktoba 9, 2021 jijini Arusha

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, ametoa medali mbalimbali jijini Arusha leo Jumamosi, Oktoba 9, 2021, kwenye kilele cha Michezo ya Riadha Kitaifa, akisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ina jambo na sekta ya michezo.

“Rais Samia ana jambo katika sekta ya michezo; Serikali yake inawekeza sana katika michezo kama sekta ya kimkakati kiuchumi, afya na utalii. Ndio maana ameongeza fedha za Timu za Taifa, ametoa asilimia 5 ya mapato ya michezo ya kubashiri matokeo kusaidia michezo na mwaka huu tunakwenda kurejesha Taifa Cup ambapo michezo itachezwa kuanzia ngazi ya wilaya na mikoa na kuja kifaifa. Uwekezaji huu umeanza kuleta tija michezoni. Tuwe wamoja tu,” alisema Dkt. Abbasi.

Ametumia fursa hiyo pia kuzitakia kheri na kuzipongeza timu mbalimbali za Tanzania ambazo wiki hii na leo zinacheza/zimetwaa ubingwa wa aina mbalimbali; Twiga Stars na Tanzanite Ladies(U20) leo zinashuka dimbani Twiga ikiwania ubingwa katika fainali za COSAFA kule Afrika Kusini na Tanzanite ikicheza na Eritrea Dar kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia.

Ameitakia kheri Taifa Stars inayoshuka uwanjani kesho nchini Benin na ameipongeza Timu ya Taifa ya Kriketi U19 ambayo imeshika nafasi ya tatu Afrika katika mashindano ya Afrika yaliyomalizika juzi nchini Rwanda.

Katika mashindano hayo Failuna Matanga kutoka Arusha ambaye  aliiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Olympik kwa mbio ndefu kwa upande wa wanawke ndiye ameibuka mshindi wa kwanza kwa mbio za mita 10000 na kufuatiwa na Natalia  Elisante kutoka Unguja na nafasi ya tatu ilichukuliwa na  Maliseline Issa  kutoka Arusha

Kwa apande wa wavulana kwa mbio hizo hizo nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Faraja Damas kutoka Arusha, wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na Inyasi Sulle kutoka Arusha na nafasi ya tatu kwenda kwa Aphonce Simbu kutoka Singida.

Kwa upande wa kurusha tufe Unguja ndiyo walioutawala mchezo huo ambapo washindi wote watatu walitoka huko. Washindi hao ni Tama Jaha Saburi aliyeshika nafasi ya kwanza, Lulu r. Kanua nafasi ya pili na Fatma Hamis aliyeshika nafasi ya tatu.

Kwa upande wa kurusha kisahani Joyce Mwang’amba kutoka Dodoma ndiye aliyeibuka mshindi wa kwanza akifuatiwa na Lulu Richard kutoka Unguja na Fatma Hamis aliyeshika nafasi ya tatu kutoka Unguja.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com