Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ameagiza kukamatwa watu wote watakaobainaka kupotosha UMMA kuhusu ukweli juu ya Sensa ya watu na makazi kwa lengo la kukwamisha zoezi hilo la kitaifa lenye faida kubwa ya maendeleo kwa taifa la Tanzania.
Akizungumza na wananchi katika nyakati tofauti kwenye Mikutano ya hadhara anayoendelea kuifanya Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa serikali haitokuwa tayari kushuhudia watu wanaopinga zoezi hilo kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mipango endelevu ya Serikali kwa wananchi wake .
Moyo alieleza kuwa mkakati wa
Serikali kupitia Sensa hiyo ya watu na makazi itakyofanyika nchi nzima mwaka 2022
ni kushuhudia kila mtu aliyepo nchini siku hiyo anahesabiwa huku akieleza lengo
mahususi la kufanya hivyo ni kutengeneza dira ya maendeleo kwa Taifa kwa kuwa
na mipango thabiti itakayoweza kufanikisha kila mwananchi kupata huduma za
msingi kwa ukaribu na ukamilifu zaidi.
Alisema kuwa kuna watu wanaojiita
wanaharakati wamekuwa wakipita maeneo mbalimbali kupotosha UMMA juu ya zoezi la
sensa ambalo limepangwa kufanyika mwakani kwa lengo la serikali kupata idadi
kamili ya wananchi wa taifa la Tanzania.
“Nawaombeni wananchi
kutowasikiliza wanaharakati hao ambao wamekuwa wanaposha wananchi wenginge juu
ya zoezi la sensa huku wakidai kuwa zoezi hilo linalengo la kukibeba chama cha
mapinduzi katika uchuguzi wa mwaka 2025 jambo ambalo sio la kweli na upotoshaji
mkubwa”alisema Moyo
Moyo alisema kuwa zoezi la sensa
halina dini wala siasa bali ni zoezi ambalo linalengo la kujua idadi ya
wananchi wa taifa la Tanzania ili kuiwezesha serikali kuandaa vizuri dira ya
taifa kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania.
Hivyo mkuu wa wilaya huyo
Mohamed Hassan Moyo aliwataka viongozi wa ngazi ya kitongoji,kijiji,kata,tarafa
na wilaya kwa ujumla kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria kwa mwananchi
yoyote atakayekuwa anapotosha kampeni ya SENSA wilayani humo.
Moyo alisema kuwa tangu taifa
la Tanzania kupata uhuru mwaka 1961 zoezi la sensa ya watu na makazi
limefanyika mara sita na mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2012 hivyo wananchi
wanatakiwa kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa makalani ambao watakuwa
wanaandikisha.
Alisema kuwa wananchi wa wilaya
ya Iringa wanapaswa kujitokeza kwa wingi na kuhamasishana kulipokea zoezi hilo
la sensa ambalo linaumuhimu mkubwa katika kupanga mipango ya kimaendeleo ya
taifa la Tanzania.
Moyo alitilia mkazo suala la
kukamatwa kwa wanasiasa na wanaharakati ambao wamekuwa wakipotosha maswala
muhimu yanayotangazwa na serikali kwa ajili ya maendeleo ya serikali
Aidha mkuu wa wilaya Moyo
aliwataka wananchi wa wilaya ya Iringa kuendelea kupata chanjo ya UVIKO 19 kama
ambavyo serikali imeagiza na kuwataka kuachana na taarifa za upotoshaji
zinazotolewa na wanasiasa na wanaharaka ambao halitakii mema taifa na wananchi
kwa ujumla.
Awali baadhi ya wananchi
walisema kuwa wamekuwa wakiambiwa na baadhi ya wanaharakati kuwa wasikubari
kuhesabiwa na kutoa taarifa zao kwa mawakara wa zoezi hilo kwa kuwa zoezi la sensa
litakuwa linafaida kwa chama chama mapinduzi (CCM) katika uchanguzi wa mwaka
2025.
Walisema kuwa wameambiwa kuwa kuanzishwa
kwa zoezi la sensa kunalengo la kuisaidia CCM kuiba kura wakati wa uchaguzi wa
serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025
Lakini mara baada ya kupokea ujumbe wa mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo baadhi ya wananchi na viongozi wa vijiji,vitongoji,kata na tarafa walisema kuwa sasa wameilewa vilivyo kampeni hiyo na wapo tayari kuendelea kutoa elimu na umuhimu wa sensa ya watu na makazi kwa ajili ya faida ya taifa.
Walisema kuwa wananchi wote wanatakiwa kuwapuuza wanasiasa na wanaharakati ambao wamekuwa wakipotosha zoezi la sensa ya watu na makazi kwa ajili ya kutengeneza dira ya taifa ya maendeleo.
0 comments:
Post a Comment