Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda amewataka wadau wa maendeleo na elimu kujitokeza kwa wingi kushirikiana na serikali ya wilaya ya Rombo ili kuboresha miundombinu ya shule kwani maendeleo hayaletwi na serikali peke yake bali kwa kushirikiana, ameyasema hayo hivi leo wakati akifanya uzinduzi wa vyoo vya kisasa vya wanafunzi na walimu shule ya msingi Mbomai juu
Waziri Mkenda ameongeza kuwa kutokana na mfano ambao umeanza kuonyeshwa na baadhi ya wadau walioshirikiana na ofisi ya mbunge wa jimbo la Rombo na Serikali katika ujenzi wa vyoo vya kisasa vya shule hiyo, umeleta mwanga na kuonyesha jinsi ambavyo wadau wakiunga mkono serikali baadhi ya changamoto katika elimu hasa miundombinu zitatatuliwa
Aidha amesema kuwa kutokana na ziara aliyoifanya wilayani hapo ameona umuhimu wa wadau kuungana na serikali kuboresha baadhi ya majengo ya shule za wilaya hiyo kwani kuna uhitaji mkubwa hasa kwenye ujenzi wa vyoo na vyumba vya madarasa
Pia Mkenda amewataka watendaji wote kuhakikisha wanaiga mfano wa ujenzi uliofanywa wa choo bora cha shule ya msingi Mbomai juu ambacho wadau na serikali wameungana na kufanikisha kujenga choo cha gharama nafuu na cha kisasa kwani ufaulu mzuri unaanzana na mazingira mazuri ya kujifunzia
“ hatutegemei kuona mwanafunzi anatoka nyumbani ambapo kuna choo kizuri alafu anafika shuleni hakuna mahali pa kujisaidia kunamfanya ashindwe kuzingatia masomo” alisema Waziri Mkenda
Waziri Mkenda amezindua choo cha shule hiyo ya Msimngi Mbomai Juu cha wanafunzi cha kisasa chenye matundu kumi na sita(16) na choo cha walimu chenye matundu mawili (2) kilicho gharimu shilingi Milioni thelethini na nne,laki tano na kumi elfu ambayo imepatikana kutokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo Mfuko wa Mbunge,halmashauri na wadau wa maendeleo
Ambapo baadhi ya vyumba vitatumiwa na wanafunzi wenye mahitaji maalumu(Walemavu) hii ni baada ya choo kilichokuwepo kupata dhuruba wakati wa mvua kali
Katika hatua nyingine waziri mkenda alitumia wasaa huo kuwahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO 19 ambayo imeanza kutolewa hapa nchini katika vituo mbalimbali vya afya
“ni watake ndugu zangu japo ni hiyari lakini twendeni tukachanje kwani ugonjwa huu ni hatari sana ana umeuwa watu wengi sana hapa jimboni kwetu” alisema Waziri Mkenda
0 comments:
Post a Comment