METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 17, 2021

MAJALIWA AMPOKEA KADA WA ACT WAZALENDO, KIGOMA

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa  akiwa ameweka simu kwenye kinasa sauti kuwawezesha washiriki wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma kumsikia Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ambaye alizungumza na wajumbe hao kwa njia ya simu wakati  kikao hicho kikiendelea  kwenye ukumbi wa CCM Mkoa, Septemba 16, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa akizungumza wakati aliposhiriki katika  Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa, Septemba 16, 2021. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba na kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mkoa wa Kigoma, Abdulkadir Mushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya washiriki wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma wakimsikiliza, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashuri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa, Septemba 16, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya CCM, Edibily Kinyoma ambaye amekihama cha ACT Wazalendo na kujiunga na CCM katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa, Septemba 16, 2021. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba na wa tatu kulia ni Katibu wa CCM wa Mkoa  Kigoma, Kajoro Vyohoroka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri kuu ya Chama cha Mapinduzi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 16, 2021 amempokea kada wa Chama cha ACT-Wazalendo  aliyekuwa mgombea wa ubunge katika jimbo la Kasulu vijijini Adibily Kazala

akizungumza baada ya kupokea kadi ya CCM  wakati wa Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kigoma Bw. Edibily amesema kuwa ameamua kujiunga na CCM ili kuweza kushikiri kikamilifu katika ujenzi wa taifa kwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za kuleta maendeleo zinazotekelezwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

amesema kuwa atashirikiana na wanachama wa CCM katika kuhakikisha juhudi za kuwafikishia watanzania maendeleo zinatekelezwa kama ilivyokusudiwa na Chama hicho.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Kassim Majaliwa amewakumbusha viongozi wa Chama hicho kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyoelekezwa katika ilani ya uchaguzi ya chama hicho.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com