METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 23, 2021

KONGAMANO LA WADAU KUHUSU UPATIKANAJI WA RASILIMALI ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI LAZINDULIWA

 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akifungua Kongamano la Wadau wa Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. Kongamano hilo limefanyika hii leo 23/09/2021 katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba, Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar na Mkurugenzi wa REPOA Dkt. Donald Mmari.

Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akihutubia wadau walioshiriki kongamano la Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. Mhe. Balozi amesisitiza kuendelea kushirikiana na Tanzania katika jitihada za kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiteta jambo na Mkurugenzi wa REPOA Dkt. Donald Mmari (kushoto) mara baada ya kufungua Kongamano la Wadau wa Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi  hii leo katika ukumbi wa Royal Village Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba.

Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akizungumza na Bw. Richard Muyungi ambaye ni Mjumbe wa Green Climate Fund kwa niaba ya Afrika, kuhusu Maandalizi ya Mkutano wa Glasgow hasa matarajio ya Afrika na Tanzania katika Mkutano huo kuhusu upatikanaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com