METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 19, 2021

WAZIRI MKENDA AITAKA CPB KUFANYA MAAMUZI KIBIASHARA ILI KUJIEPUSHA NA ANGUKO KAMA TAASISI ZILIZOTANGULIA

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Wa Pili Kushoto) akizindua Viwanda viwili cha kusaga mahindi na kuchakata alizeti vilivyopo ofisi za Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) eneo la Kizota Jijini Dodoma, jana tarehe 19 Agosti 2021. Wengine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe Jabir Shekimweri (Wa Kwanza KUshoto), Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe Antony Mavunde (Wa Pili Kulia) na Mkurugenzi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Dkt Anslem Moshi (Wa kwanza kulia). (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Viwanda viwili cha kusaga mahindi na kuchakata alizeti vilivyopo ofisi za Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) eneo la Kizota Jijini Dodoma, jana tarehe 19 Agosti 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Viwanda viwili cha kusaga mahindi na kuchakata alizeti vilivyopo ofisi za Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) eneo la Kizota Jijini Dodoma, jana tarehe 19 Agosti 2021.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akikagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) wakati wa uzinduzi wa Viwanda viwili cha kusaga mahindi na kuchakata alizeti vilivyopo ofisi za Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) eneo la Kizota Jijini Dodoma, jana tarehe 19 Agosti 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akikagua ufanyaji kazi wa kiwanda cha kuchakata alizeti wakati wa uzinduzi wa Viwanda viwili cha kusaga mahindi na kuchakata alizeti vilivyopo ofisi za Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) eneo la Kizota Jijini Dodoma, jana tarehe 19 Agosti 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akionyesha zawadi ya unga bora wa mahindi unaozalishwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) wakati wa uzinduzi wa Viwanda viwili cha kusaga mahindi na kuchakata alizeti vilivyopo ofisi za Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) eneo la Kizota Jijini Dodoma, jana tarehe 19 Agosti 2021.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

 

Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda ameitaka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) kuhakikisha inafanya maamuzi yake kibiashara ili kujiepusha na anguko lililozikumba taasisi zilizotangulia.


Prof. Mkenda ameyasema hayo jana tarehe 19 Agosti 2021 wakati akizindua Viwanda viwili cha kusaga mahindi na kuchakata alizeti vilivyopo ofisi za CPB eneo la Kizota Jijini Dodoma.


Amesema Taasisi zilizokufa za General Agricultural Products and Exports Board (GAPEX) na National Milling Corporation (NMC) ilitokana na kufanya maamuzi mengi kufanyika kwa misingi isiyokuwa ya kibiashara.


"Mwelekeo ni mzuri umenipa matumaini kwamba hamtashindwa tena kama kwenye National Milling na GAPEX, "alisema Prof. Mkenda.


Amefafanua zaidi ya kuwa serikali itazidi kuwa pamoja na bodi hiyo ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika masuala ya usimamizi wa mazao ili kuleta matokeo chanya.


Hata hivyo, ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inatekeleza suala la kuingia kwenye mkataba na wakulima wakubwa na wadogo wa kilimo cha alizeti ambao watajiunga kwenye ushirika ili kusaidia kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula nchini.


Amesema kuwa wakifanya hivyo wao, serikali itasimamia katika suala zima la Maafisa ugani na kuzalisha mbegu bora za alizeti ambazo zitatoa mafuta kwa wingi.


Amewataka wakulima kutumia fursa hiyo ya CPB kulima mashamba makubwa yatakayo wawezesha kuingia kilimo cha mkataba na bodi hiyo ili kufanya Kilimo chenye tija.


Akizungumzia suala la mahindi, amesema CPB wanapaswa kutangaza soko la mahindi nje ya nchi kwa sababu mahindi ya Tanzania hayana Sumukuvu. 


Waziri Mkenda amesema kuwa CPB wanapaswa kusimama imara kuhakikisha wanatangaza soko kwa sababu wamekagua mahindi na kuona yana kila aina ya sifa na ubora wa kuuzwa popote.


Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa CPB, Dkt Anselm Moshi, amesema viwanda ambavyo wamezindua cha mahindi kina uwezo wa kusaga tani 60 kwa siku huku cha Alizeti tani 40 kwa siku.


Aidha, amesema viwanda hivyo wametumia jumla ya Tsh Bilioni 7.092 ambapo fedha nyingine wamepata mkopo kutoka NSSF.


MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com