METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, August 2, 2021

WAZIRI BASHUNGWA AWATAKA BAKITA KWENDA NA KASI YA KUKUA KWA TEKNOLOJIA ILI KUTANGAZA KISWAHILI DUNIANI



WAZIRI BASHUNGWA AWATAKA BAKITA KWENDA NA KASI YA KUKUA KWA TEKNOLOJIA ILI KUTANGAZA KISWAHILI DUNIANI. 

“Bakita amkeni achaneni na njia za kizamani tumieni njia za kielekroniki sasahivi ulimwengu umehama upo mtandaoni, idara ya Tehama kazeni buti, mtu wa nchi za nje atapataje machapisho yenu kama hamuwekei mkazo katika kutoa taarifa kupitia mitandao?” Amesema Bashungwa.

 

Waziri Wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ametoa maagizo hayo leo Agosti 2, 2021 Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika ofisi za Baraza la Kiswahili Nchini (BAKITA) na kuwaagiza kuanza kutumia njia mpya yakujitangaza na kutangaza kiswahili nchini na kuachana na mifumo ya kizamani na pia kuangalia fursa za kuanzisha vituo vya mafunzo ya kiswahili katika Balozi zetu mbali mbali Duniani ili Kuunganisha Kiswahili na utalii kukuza kiswahili pamoja na Utamaduni wa Tanzania.

 

Katika ziara hii Mhe. Bashungwa alitembelea darasa la kisasa la kufundishia wakalimani lililofunwa vifaa vya kisasa ambalo bado halijafunguliwa rasmi kwa sasa, vile vile kwa upande wa BAKITA wamemuelezea Mhe. Waziri mipango yao ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 wakuongeza idadi ya wakalimani 50 nchini ili kukidhi hitaji la ukalimani ili kukidhi tija ya huduma hii nchini.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com