METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 14, 2021

MWENYEKITI WA WAZAZI CCM MUFINDI FESTO KILIPAMWAMBU AHIMIZA WANANCHI KWENDA KUPATA CHANJO YA COVID 19

Mwenyekitiwa Jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi  Festo Kilipamwambu akiongea na wajumbe wa baraza la wazazi wa jumiya hiyo.Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi James Mgego akiongea na wajumbe wa baraza la wazazi la jumiya ya chama cha mapinduzi wilaya ya MufindiBaadhi Wajumbe wa baraza la wazazi wa jumuiya ya chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi

Na Fredy Mgunda,Iringa. 

JUMUIYA ya wazazi ya chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi imewataka wananchi na wanachama wa chama hicho kuakikisha wanaenda kupata chanjo ya COVID 19 kwa lengo la kujikinga na ugonjwa wa Corona. 

Akizungumza  kwenye baraza la jumuiya ya wazazi wa chama hicho,mwenyekitiwa Jumuiya hiyo Festo Kilipamwambu alisema kunahaja ya wajumbe wa jumuiya hiyo kwenda kupata chanjo hiyo kwa lengo la kujikinga kutoka na kuwa na umri mkubwa. 

Aliwataka wananchama wa jumuiya hiyo kuzipuuza habari za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu juu ya chanjo hiyo ambayo inasaidia kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Corona. 

Kilipamwambu alisema kuwa ugonjwa wa Corona upon a unaua hivyo ni bora kuchukua tahadhari ya kupata chanjo ambayo inasaidia kujikinga na ugonjwa huo ambao umekuwa janga kubwa la dunia kwa ujumla. 

“Naowaombeni sana wajumbe wa jumuiya hii ya wazazi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi kuhakikisha mnaenda kupata chanjo ya COVID 19 kwa lengo la kulinda afya zetu na kufikisha ujumbe tuliwapa kwa wananchi wengine ambao hawaamini kuwa chanjo hiyo ni muhimu kwao” alisema Kilipamwambu 

kwa upande wake Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi James Mgego aliwataka viongozi wa jumuiya ya wazazi wa chama hicho kuhakikisha wanafika kwenye vikao husika kwa lengo la kukijenga chama. 

Alisema kuwa walichaguliwa kwa lengo la kuhakikisha wanawawakilisha wanachama wengine kwenye vikao kuanzia ngazi ya tawi hadi wilaya kwa lengo la kukijenga chama. 

Mgego aliwataka wajumbe wa jumuiya ya wazazi kuhakikisha wanahudhuria vikao vyote vya chama kwa kufikisha maono ya wanachama wengi ambao hawawezi kuhudhuria vikao vya wilaya. 

Alisema kuwa anaipongeza jumuiya ya wazazi kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakiksha wanakijenga chama na kufanikisha ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka 2020 kwa kushinda nafasi zote.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com