Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa wakati apokutana na kuzungumza nao katika kikao kazi wilayani humo katika Mkoa wa Dodoma, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Leo tarehe 17 Agosti 2021. Wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Antony Mtaka (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Renidius Mwema. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa wakati apokutana na kuzungumza nao katika kikao kazi wilayani humo katika Mkoa wa Dodoma, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Leo tarehe 17 Agosti 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Antony Mtaka wakimkabidhi zawadi ya Televisheni Afisa Ugani Kata ya Ng'humbi Ndg Charles Mujule kama kielelezo cha kufanya kazi kwa ufanisi wakati alipokutana na kuzungumza na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa katika Mkoa wa Dodoma, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Leo tarehe 17 Agosti 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Antony Mtaka (Kulia) akizungumza na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa katika kikao kazi wilayani humo katika Mkoa wa Dodoma, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Leo tarehe 17 Agosti 2021. Wengine pichani ni Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Renidius Mwema (Kushoto).
Sehemu ya maafisa Ugani wa wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) wakati wa kikao kazi kilichofanyika Leo tarehe 17 Agosti 2021 katika ofisi za Halamshauri ya Wilaya ya kongwa.
Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Antony Mtaka (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Renidius Mwema (Katikati) wakizungumza mara baada ya kikao cha kazi na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Leo tarehe 17 Agosti 2021.
Sehemu ya maafisa Ugani wa wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) wakati wa kikao kazi kilichofanyika Leo tarehe 17 Agosti 2021 katika ofisi za Halamshauri ya Wilaya ya kongwa.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kongwa
Waziri
wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) amesema kuwa Wizara ya Kilimo ilifanya
utafiti ikagundua kuwa ili iweze kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta
ya kilimo ni wazi kuwa lazima kuwatumia maafisa ugani kwa umuhimu na ufanisi mkubwa.
Amesema
kuwa maafisa ugani ndio mboni ya jicho la Wizara ya Kilimo hivyo ili nchi iweze
kuwa na kilimo bora kinachokidhi matakwa ya tija na wingi wa uzalishaji na kuwa
na kilimo kitakachokidhi matakwa ya soko ni wazi kuwa elimu ni muhimu itolewe
kwa wakulima.
Waziri
wa Kilimo ameyasema hayo leo tarehe 17 Agosti 2021 wakati akizungumza kwenye
kikao kazi na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa akiwa katika ziara ya kikazi ya
siku moja wilayani hapo mkoani Dodoma.
Amesema
kuwa serikali imeandaa mafunzo rejea kwa maafisa ugani wote nchini ili
kuimarisha sekta ya kilimo na kila afisa ugani katika mikoa kielelezo ya
Dodoma, Singida na Simiyu atakabidhiwa Pikipiki kwa ajili ya kurahisisha huduma
zao kwa kuwafikia wakulima wengi kwa siku.
Ameongeza
kuwa pamoja na pikipiki hizo kwa maafisa ugani, pia serikali itawapatia simu za
mkononi kwa ajili ya kurahisisha huduma za mawasiliano na wakulima ikiwa ni
pamoja na kuzitumia kwa ajili ya taarifa za utendaji kazi wao.
Pia,
ameongeza kuwa maafisa ugani wote wanapaswa kuwa na mashamba ya mifano ambayo
serikali itaandaa mfumo mzuri kwa ajili ya kuwasaidia pembejeo ili wawe
kielelezo kizuri kwa wakulima katika maeneo yao.
“Mimi
nikitaka kujua kama kweli afisa ugani anafanya kazi yake inavyotakiwa nikienda
kwenye eneo lake si nitaomba tu kuona shamba lake alilolima kisha
nitajiridhisha kwamba anafaa” Amekaririwa Waziri Mkenda
Kuhusu
kilimo cha alizeti Waziri Mkenda amesema kuwa maafisa ugani wengi wamekuwa
wakifanya kazi zisizohusiana na kilimo lakini serikali ipo katika mkakati wa
kuwarejesha kwenye majukumu yao ili kuongeza kasi ya kukuza kilimo nchini.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment