METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, August 13, 2021

COSOTA YAELEZA DHAMIRA YA KUFANYA TOZO ZA MIRABAHA KUWA ZENYE UWEZO WA KULIPIKA

Mwanasheria wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Lupakisyo Mwambinga akizungumza na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa kuhusu lengo la kukusanya maoni ya wadau kwa rasimu ya Kanuni ya Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa Umma ya mwaka 2021 ambapo amesisitiza maoni ya wadau hao kuzingatiwa leo Agosti 11,2021 Jijini Mwanza. 

Mwanasheria wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Lupakisyo Mwambinga akizungumza na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa (hawapo pichani) kuhusu lengo la kukusanya maoni ya wadau kwa rasimu ya Kanuni ya Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa Umma ya mwaka 2021 ambapo amesisitiza maoni ya wadau hao kuzingatiwa leo Agosti 11,2021 Jijini Mwanza.

Muwakilishi wa Mmiliki wa Sahara Media Stephen Diallo akitoa maoni  ya kuomba COSOTA kuacha tozo za mirabaha kuwa za kiwango cha shilingi laki tano na laki tatu kama ilivyokuwa awali badala ya kiwango kilichopo kwenye rasimu ya Kanuni ya Leseni na Maonesho kwa Umma ya mwaka 2021 leo Agosti 11, 2021 Jijini Mwanza katika kikao cha kuwasilisha maoni . 

Muwakilishi wa KISS FM Sharbano Ally  akitoa maoni  ya COSOTA kutoa taarifa ya namna imegawa mirabaha ya awali ili kuweka kwa uwazi hilo kwa wadau wanaolipa tozo hiyo kwenye kikao cha kukusanya maoni ya rasimu ya Kanuni ya Leseni na Maonesho kwa Umma ya mwaka 2021 leo Agosti 11, 2021 Jijini Mwanza. 

Muwakilishi wa Mmiliki Vision FM Aron Peter kutoka Kagera akiomba kuomba COSOTA kuondoa tozo ya mirabaha kwa vyombo vya habari  kwani tozo hizo zitapelekea vyombo kumlipisha mwanamuziki ili wimbo wake upigwe kwenye redio kwa lengo la kuweza kupata pesa ya kulipa mirabaha hiyo, leoAgosti 11, 2021 katika kikao cha kukusanya maoni ya Kanuni ya Leseni ya Utangazaji na maonesho kwa umma 2021.

Anitha Jonas – COSOTA, Mwanza

Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) yawatoa wasiwasi wamiliki wa vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa kwa kusema kuwa maoni yote wanayotoa kuhusu tozo ya mirabaha kwa rasimu ya Kanuni ya Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa Umma ya mwaka 2021 kuwa yatafanyiwa kazi.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 11,  2021 Jijini Mwanza na Mwanasheria wa COSOTA Lupakisyo Mwambinga katika kikao cha kukusanya maoni ya rasimu ya Kanuni ya Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa Umma kilicholenga kupata maoni ya tozo za mirabaha zilizopangwa kwa matumizi ya Muziki katika vyombo vya habari.

“Maoni yote tumeyapokea na tutayafikisha panapohusika na kwa wadau wa kebo tumepokea maoni yenu na changamoto zenu tutaziwasilisha ofisini ili zifanyiwe kazi na naomba mfahamu ya kuwa kikao hichi kimelenga kujenga mazingira rafiki ya tozo hii ya mirabaha iweze kulipika,” alisema Mwambinga.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Mwanasheria huyo wa COSOTA alisisitiza kuwa Kanuni hiyo ni rasimu na hivyo maoni ya wadau ndiyo yataiboresha na kuifanya iweze kutekelezeka.

Pamoja na hayo nae Msimamizi wa Kituo cha Bunda FM Revocatus Andrew aliiomba COSOTA kupunguza tozo hizo na kurudisha kiasi cha zamani ambapo walilipa laki tatu na wengine laki tano, kwani  tozo ya milioni moja na nusu ni pesa nyingi kulingana na hali ya uchumi ilivyosasa hivyo akaisisitiza taasisi hiyo kuzingatia maoni hayo wanayotoa na kuyafanyia kazi.

“Jamani biashara ya redio kwa sasa ni ngumu sana na tunajiendesha kwa tabu hayo matangazo mnayozungumzia kwa sasa hayapatikani inafikia wakati hata pesa ya umeme wa kuendesha kituo ni changamoto halikadhalika mishahara ya wafanyakazi naomba COSOTA hili mliangalie vizuri,” alisema Andrew.

Halikadhalika kwa upande wamiliki wa Kebo Mmiliki wa Barmedas Com Ltd Hussein Hassan wa Jijini Mwanza aliomba COSOTA kushusha gharama za tozo hiyo ya mirabaha kwa Kebo televisheni kupendekeza ishushwe mpaka laki moja badala ya shilingi milioni moja na nusu iliyopendekezwa katika rasimu hiyo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com