Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Prof.
Adolf Mkenda Leo tarehe 4 Juni 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Mhe Antony Mtaka akiwa ameambatana na wataalamu wa sekta ya
Kilimo ambapo miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na kutafuta ufumbuzi
wa changamoto ya uagizaji wa mafuta ya kula.
Waziri Mkenda amesema kuwa
tarehe 13 Juni 2021 Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika mkutano wa kuhamasisha kilimo cha alizeti mkoani Singida ikiwa ni
njia mojawapo ya kuikabili changamoto ya uagizaji wa mafuta ya kula nje ya
nchi.
Waziri Mkenda ameongeza kuwa serikali itaianza safari yake kwa
kuboresha huduma za ugani katika mikoa mitatu ya kielelezo ambayo ni Dodoma, Singida
na Simiyu kwani Mikoa hiyo ina fursa kubwa ya kuzalisha mazao ya mafuta hususani
alizeti na pamba na hivyo itaongeza chachu kubwa ya uzalishaji Alizeti ikiwa ni
hatua nzuri kuelekea upatikanaji wa mafuta ya kutosha.
“Tutaanzisha kampeni ya
wakulima wakubwa, AMCOS na wakulima wote nchi nzima, Tutawafungamanisha na
wanaozalisha mafuta ya alizeti ili wapate mikataba, tutahakikisha wanapata
mbegu za kutosha kuhakikisha wanazalisha alizeti” Amekaririwa Prof Mkenda
Katika hatua nyingine Waziri
Mkenda amempongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma kwa usimamizi madhubuti katika
sekta ya kilimo na kutoa kipaumbele kikubwa katika utekelezaji wa Bajeti ya
Wizara ya Kilimo yam waka 2021/2022.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mhe Antony Mtaka amesema kuwa timu hiyo ya Mkoa wa Dodoma aliyoingoza
katika kikao hicho na Waziri wa Kilimo imekusudia kujibu utekelezaji wa hotuba
ya Wizara ya Kilimo yam waka 2021/2922 kuhusu kukabiliana na changamoto ya
uagizaji wa mafuta ya kula nje ya nchi.
Amesema kuwa mkoa wa Dodoma
kupitia Wilaya zinazozunguka Jiji la Dodoma za Kongwa, Chemba na Kondoa ambazo
ni wazalishaji wakubwa wa zao la Alizeti wanaingia katika jawabu la kukabiliana
na changamoto ya tija ndogo katika uzalishaji wa alizeti pamoja uagizaji wa
mafuta ya kula.
“Na sisi kama mkoa
tungehitaji tuwe na uwezo wa kuzalisha alizeti kwa tija na kuona namna ambavyo Block
Farming inaweza kufanyika kwa ufanisi na namna ambavyo wakulima wetu
wadogo wadogo tunaweza kuwafikia ili yale malengo ya wizara yaweze kufanikiwa
kwa unafuu zaidi” Amekaririwa Rc Mtaka
Mhe Mtaka amesema kuwa lazima
ifike mahala hata kama uagizaji wa mafuta nje ya nchi utaendelea lakini nchi
nayo iwe na uhakika wa kuzalisha mafuta kwa wingi ikiwa ni pamoja na kuuza nje
ya nchi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment