METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 4, 2021

WAZIRI JAFO AZINDUA MPANGO MKAKATI WA TAIFA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo,akizungumza wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Hassan Chande,akizungumza wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Marry Maganga ,akizungumza wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui,akitoa neno wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa  Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.

 

 

Baadhi ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na kuzindua Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo akizindua   Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi mara baada ya kufungua Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevupamoja na kuzindua Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo akimkabidhi kitabu cha Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui mara baada ya kufungua Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo,amezindua Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 huku akiitaka jamii kuishi kwa kufuata misingi ya ajenda za kimazingira.

 Akizungumza katika uzinduzi huo sambamba na kufungua Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu Mhe.Jafo amesema kuwa Mkakati huo utasaidia kuondokana na uharibifu wa mazingira uliopo kwa sasa uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.

Waziri Jafo amesema kuwa Kutokana na mapinduzi ya viwanda na shughuli za kibinadamu zimeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia nchi na kuipa changamoto Dunia Katika kutafuta suluhu za kimazingira.

“Bila kulinda mazingira, dunia haitokuwa sehemu salama na uchumi wa mataifa mengi utadidimia hivyo Kuna haja kwa nchi zilizoendelea kuzisaidia nchi masikini kupambana na athari za kimazingira, zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi,”amesema Mhe.Jafo

Amesema kuwa  wataalamu wanasema asilimia moja ya pato la Taifa linapotea kila mwaka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi pia ikikadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 wa ukanda wa pwani watakabiliwa na changamoto za Mazingira ifikapo mwaka 2030 ikiwa jamii haitaacha shughuli za kibinadamu zinazoathiri mazingira.

Pia ametaja athari moja wapo ambayo imetokana na Mabadiliko ya tabianchi na kusema kuwa maji ya ziwa Tanganyika yameongezeka na kufikià mita mbili Jambo ambalo si salama kwa maisha ya binadamu.

“Tusiposimama pamoja Katika kutekekeza ajenda ya mazingira dunia yetu haitakuwa salama,wavuvi wanapaswa pia kuvua kwa kutumia zama zinazokibaliwa ili kulinda viumbe wa majini,”amesema Jafo

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Marry Maganga, amesema kuwa uzinduzi huo umekwanda pamoja na uwasilishwaji mada kuhusu matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza matumizi ya misitu.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui,ameipongeza serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kwa kuwa na ushirikiano mzuri katika suala zima la kuhamasisha jamii utunzaji wa mazingira kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com