WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo,akizungumza wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Hassan Chande,akizungumza wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Marry Maganga ,akizungumza wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui,akitoa neno wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na kuzindua Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo akizindua Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi mara baada ya kufungua Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevupamoja na kuzindua Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Selemani Jafo akimkabidhi kitabu cha Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui mara baada ya kufungua Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu pamoja na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo,amezindua Mpango Mkakati wa Taifa wa
kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 2021 hadi 2026 huku akiitaka jamii
kuishi kwa kufuata misingi ya ajenda za kimazingira.
Akizungumza katika uzinduzi huo
sambamba na kufungua Kongamano la hifadhi ya Mazingira na Maendeleo Endelevu
Mhe.Jafo amesema kuwa Mkakati huo utasaidia kuondokana na uharibifu wa
mazingira uliopo kwa sasa uliofanyika leo June 4,2021 jijini Dodoma.
Waziri Jafo amesema kuwa Kutokana na
mapinduzi ya viwanda na shughuli za kibinadamu zimeweza kuchangia kwa kiasi
kikubwa mabadiliko ya tabia nchi na kuipa changamoto Dunia Katika kutafuta
suluhu za kimazingira.
“Bila kulinda mazingira, dunia haitokuwa
sehemu salama na uchumi wa mataifa mengi utadidimia hivyo Kuna haja kwa nchi
zilizoendelea kuzisaidia nchi masikini kupambana na athari za kimazingira,
zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi,”amesema Mhe.Jafo
Amesema kuwa wataalamu wanasema
asilimia moja ya pato la Taifa linapotea kila mwaka kutokana na mabadiliko ya
tabia nchi pia ikikadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 wa ukanda wa pwani
watakabiliwa na changamoto za Mazingira ifikapo mwaka 2030 ikiwa jamii
haitaacha shughuli za kibinadamu zinazoathiri mazingira.
Pia ametaja athari moja wapo ambayo
imetokana na Mabadiliko ya tabianchi na kusema kuwa maji ya ziwa Tanganyika
yameongezeka na kufikià mita mbili Jambo ambalo si salama kwa maisha ya
binadamu.
“Tusiposimama pamoja Katika kutekekeza
ajenda ya mazingira dunia yetu haitakuwa salama,wavuvi wanapaswa pia kuvua kwa
kutumia zama zinazokibaliwa ili kulinda viumbe wa majini,”amesema Jafo
Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira, Marry Maganga, amesema kuwa uzinduzi huo umekwanda
pamoja na uwasilishwaji mada kuhusu matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza
matumizi ya misitu.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania Bi.Haika Mtui,ameipongeza serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kwa kuwa na ushirikiano mzuri katika suala zima la kuhamasisha jamii utunzaji wa mazingira kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi.
0 comments:
Post a Comment