Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zimetiliana saini mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na shilingi bilioni 361.71 kwa ajili ya kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa jua Megawatt 150 Wilaya ya Kishapu,Shinyanga.
Mradi huu ni wa mwaka mmoja ambao unatarajiwa kuanza mwezi machi 2022 na kukamilika mwezi Machi 2023.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba wakati wa kusainiwa kwa mkataba wa mkopo huoJijini Dodoma.
"Mradi huu unatarajiwa kuwa wa awamu mbili ambapo tunaanza na awamu ya kwanza itakayoweza kuzalisha Megawatt 50 na sehemu ya fedha za mkopo huu zitatumika kuboresha na kuimarisha Grid ya Taifa kuifanya ya kisasa kuweza kujumuisha umeme wa nishati jadidifu zenye muda maalum na pia kupunguza upotevu wa umeme"Alisema Tutuba
Akizungumzia faida za mradi huo amesema mradi huu utaongeza uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme ili kuiwezesha TANESCO kutimiza malengo ya kuzalisha umeme kupitia vyanzo mbalimbali kwa kutumia Nishati jadidifu
Aidha Mradi huu utapungua utegemezi wa umeme wa nguvu za maji wakati wa maji wakati wa jua, hivyo kuwa na uwezo wa ziada za uzalishaji ambao utatumika majira ya mahitaji makubwa ya umeme na wakati wa ukame.
Amesema nyongeza hiyo ya Megawatt 150 ya umeme wa jua pindi mradi utakapokamilika utawezesha upatikanaji wa umeme katika migodi ya dhahabu na kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme katika gridi ya Taifa.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt Titto Mwinuka ambaye alikuwa akimwakilisha Katibu Mkuu Nishati amesema mradi huo utachangia kwenye lengo la Taifa la kufikisha Megawatt 5000 kufikia mwaka 2025
"Mradi huu utatuwezesha kuwa na mchanganyiko mkubwa zaidi wa vyanzo vya nishati nchini kwa sababu lengo ni kutotegemea chanzo kimoja kwa sababu hatujawahi kuwa na chanzo cha jua katika vyanzo vyetu vya umeme"alisema Mwinuka
Amesema chanzo hiki cha jua ni rahisi kupatikana tofauti na vyanzo vya maji na Nyuklia ambapo kwani unit 1 itapatikana kwa bei ya chini ya shilingi 103.5 ambayo ni bei ya chini sana na pia nguvu ya jua ni rafiki wa mazingira kwaiyo kwenye utekelezaji hakutakuwa na athari katika mazingira.
Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Bw.Frederic Clavier amesema Tanzania inaweza kuwa mfano katika Bara la Afrika katika matumizi haya ya Nishati ya jua, na hivyo wamefurahi kuwa katika uwanja mmoja na Tanzania katika kupambania masuala ya Mabadiliko ya Hali ya hewa.
Aidha kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa AFD amesema programu hii lengo lake kubwa ni kusapoti mipango ya kitaifa ya Nishati kwa kuangalia mipango mbalimbali kwa kuwa matumizi ya nishati ya jua yanaogezeka nchini.
0 comments:
Post a Comment