Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akifafanua namna gani ambavyo anazushiwa tuhuma za kumiliki shamba Isupilo na eneo la Rodrick Mahenge
Eneo la marehemu Rodrick Mahenge ambalo pia linamgogoro baina ya familia hiyo na wapagaki wa eneo hilo
Eneo la marehemu Rodrick Mahenge ambalo pia linamgogoro baina ya familia hiyo na wapagaki wa eneo hilo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa
amekanusha tuhuma za kuchangia mgogoro wa wananchi wa kijiji cha Isupilo na
muwekezaji kampuni ya Overland mgogoro wa familia ya marehemu Rodrick Mahenge na
wapangaji wake wanaogomea kulipa kodi ya pango waliopanga katika eneo la
familia hiyo lilolopo Ipogolo Manispaa ya Iringa.
Akizungumza na viongozi wa
kijiji cha Isupilo, mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa
tuhuma zinazoenezwa na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Isupilo kuwa anachochea
mgogoro huo sio za kweli.
Alisema kuwa kumekuwa na
taarifa zinazosema kuwa anashamba la kufugia mifugo aina ya mbuzi katika shamba
hilo lenye mgogoro baina ya wananchi na muwekezaji wa kampuni ya Overland.
Kasesela alisema kuwa alienda
katika kijiji hicho kwa lengo la kutatua mgogoro huo ulikuwa umemfikia mezani
kwake kama kiongozi na sio kumpendelea mtu yeyote yule.
Alisema kuwa shamba la
muwekezaji kampuni ya Overland linahekari 1262 huku hekari 953 hazina mgogoro
wowote na hekari 296 ndio zinamgogoro ambao kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha
tuhuma hizo.
“Mimi sifugi mbuzi wa sina
shamba katika kijiji cha Isupilo nashangaa tu natuhumiwa na baadhi ya wananchi
kuwa namiliki shamba na kufuga mbuzi kitu ambacho ni uongo mkubwa amboa mimi
naukataa kabisa” alisema Kasesela
Kasesela alimalizia kwa kusema
kuwa lengo lake ni kuhakikisha anatatua mgogoro huo kwa amani ili kila mmoja
apate haki zake bila kumpendelea mtu yeyote yule.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
kijiji cha Isupilo Joachim Kisinini alisema kuwa mgogoro upo kati ya baadhi ya
wananchi na muwekezaji na sio kweli kuwa mkuu wa wilaya ya Iringa anachochea
mgogoro huo kwa manufaa yake.
Alisema kuwa shamba hilo lina
hati ya mwaka 1929 na lilikuwa linamilikiwa na Rashid Kivike kwa kipindi hicho
chote hadi pale alipoamua kuliuza kwa kampuni ya Overland na ndipo mgogoro
ulipoibuka baina ya muwekezaji huyo na wananchi ambao wanaishi na kufanya
shughuli za kilimo katika shamba hilo.
Kisinini alisema kuwa eneo la
hekari 296 ndio linamgogoro baina ya wananchi na muwekezaji na ndio mkuu wa
wilaya ya Iringa yupo kwenye mpango wa kuhakikisha anatatua mgogoro huo.
Aidha Kisinini alimalizia kwa
kusema kuwa uongozi wa kijiji hicho hawaitambui hati hiyo kutokana na mmiliki
wa awali Rashid Kivike kutolalamika mahali popote pale wakati wananchi wengine
wakiendelea kufanya shuguli za kimaendeleo katika shamba hilo.
Alisema hadi hivi sasa
muwekezaji anatumia hekeri 953 kwa shughuli zake na hizo nyingine hazitumii kwa
kuwa zinatumiwa na wananchi licha kuwa bado kunamgogoro.
Katika mgogoro mwingine mkuu wa
wilaya amekanusha kuhusu katika mgogoro wa familia ya Marehemu Rodrick Mahenge
na wapangaji wake kwa kutengeneza tuhuma kuwa amejigawia eneo kwenye eneo hilo
la familia hiyo.
Akizungumza na wasimamizi wa mirathi,
Kasesela alisema kuwa lengo lake ni kuhakikisha anatatua mgogoro huo kwa amani
na kuwaamuru wapangaji wote wanatakiwa kulipa kodi kwa wakati na wasipolipa
wanatakiwa kuondolewa haraka iwezekanavyo.
Kwa upande wake Jeny mahenge
alisema kuwa kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya familia na baadhi ya
wapangaji ambao wamekuwa wanagoma kulipa kodi toka mwaka 2017 hadi hivi sasa.
Alisema kuwa familia imekuwa
hainufaiki na chochote kile kutokana kutolipwa kwa kodi na wapangaji hao
kukaidi kulipa kodi hizo.
Lakini pia alikanusha kuwa mkuu wa wilaya Iringa Richard kasesela hana eneo analomiliki katika eneo hilo la marehemu Rodrick Mahenge kama inayosemwa huko mitandaoni na mitaani na watu wasiojua chochote kile.
0 comments:
Post a Comment