METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, June 8, 2021

Shirika la Envirocare lashiriki maadhimisho wiki ya mazingira,latoa elimu


Baadhi ya wananchi wakiwa katika banda la Envirocare wakipata Elimu kuhusu utunzaji wa mazingira 

Na Joyce Kasiki,Dodoma

SHIRIKA lisilo la Kiserikali limeiomba Serikali iendelee kutoa elimu ya mazingira ili iwajibike ipasavyo katika suala zima la utunzaji wa mazingira na kurudisha uoto wa asili nchini iliopotea kutokana na uharibifu wa mazingira.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki katika maadhimisho ya siku ya Mazingira yaliyofanyika Kitaifa mkoani hapa na Afisa Mazingira wa
Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na utoaji elimu kuhusiana na masuala mbalimbali likiwemo suala la utunzaji wa mazingira (Envirocare )Eufransia Shayo huku akisema,jamii inao wajibu mkubwa katika

kutunza mazingira kuanzia katika maeneo wanayoishi hivyo bado elimu inahitajika kwao.

“Jamii nayo inapaswa itoe ushirikiano kwa Serikali katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama”amesema Shayo

Amesema,kwa upande wa shirika hilo linaendelea kushirikiana na Serikali na lipo tayari kuhakikisha elimu hiyo inawafikia wananchi kikamilifu.

Aidha amesema,katika kuhakikisha elimu inafika kikamilifu kwa jamii,Eviorocare linafika mpaka mashuleni kutoa elimu kuanzia kwa wanafunzi wa darasa la awali katika shule za msingi mpaka shule za sekondari na vyuo.

Kuhusiana na ushiriki wao kwenye maonyesho hayo alisema,wameshiriki kikamilifu katika kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi waliofika kwenye banda lao pamoja na kugawa vipeperushi kwa wananchi vyenye ujumbe wa utunzaji wa mazingira.

“Shirika  letu linashirikiana na taasisi mbalimbali kuhakikisha elimu ya utunzaji mazingira inasambaa kuanzia kwa watoto wadogo mashuleni ili kuwajengea desturi ya kutunza mazingira tangu wakiwa wadogo,lakini

pia kuwaelimisha wananchi kwa ujumla kuwa suala la utunzaji wa mazingira ni suala la kila mtu.”amesema Shayo na kuongeza kuwa “Katika utoaji wa elimu tunafika hadi mashuleni kuwafundisha wanafunzi masuala yahusuyo  mazingira na kufanya shugjhuli mbalimbali za utunzaji mazingira mashuleni.”

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com